LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA TAYONEHO ORGANIZATION.

 Kutokana na kushuka kwa Elimu Tanzania Tayoneho kama shirika la vijana Tanzania linakuja na project ya MOBILE LIBRARY. Project hii inalenga wanafunzi wa ngazi zote za elimu kuanzia elimu ya awali nikimanisha elimu ya msingi na kwenda sekondari mpaka elimu ya juu nikimanisha chuo.

Kwa kutumia mchango wa kitabu utakachoweza kuchangia sisi kama shirika tutaweza kuazimisha vitabu hivyo kwa watu watakao kuwa na uhitaji. Vitabu hivyo vitasambazwa katika sehemu mbali za mkoa wa Mwanza kwa kuanza na badae kwenda nchi nzima.

Katika system hii mwanafunzi kwa kutumia computer yake ama simu ya mkononi ataweza kuangalia kitabu anachohitaji na center gani iliyokaribu nae kwenye system database yetu ili aweze kwenda kuazima na kujisomea kwa muda na badae aweze kurudisha.

Ni wajibu wetu sote kama watanzania kujenga taifa lililoelimika, na ili kufanikisha hilo kitabu chako kimoja kinahitajika kujenga Tanzania hiyo.

KWA PAMOJA TUNAWEZA

Kwa maelezo zaidi juu ya Project hii, wasiliana nasi kwa kutumia: Ama kwa barua pepe: tayonehotz@gmail.com
 

Imani Tinda E-mail: imanitinda@yahoo.com Phone No:+255 754 214020

Albert Deogratias E-mail:albertdeo@gmail.com Phone No:+255 684 545923

Faraji E-mail: fula5@yahoo.com Phone No:+255 713 392336

Nathern Majukano E-mail:mjaphet@yahoo.com phone:+255 658 836431

Nasir Shaban Phone No:+255 754 310213

No comments:

Powered by Blogger.