LIVE STREAM ADS

Header Ads

DADA UKIPIGA HUU MKOROGO UTABAKI NJIA KUU, HATAPATIKANA PLAYBOY WA KUKUFANYA MCHEPUKO.

Dawa ya Mchepuko.

Unataka Kubaki Njia Kuu? Basi kwa leo wewe mwana dada nataka nikupe njia itakayo kuhakikishia uhakika wa Kubaki Njia Kuu. Fanya hivi chagua mmoja wa wanaume/ wavulana ambao wamewahi kukutaka kimapenzi ama hata kutumia kigezo cha kukuoa.


Omba kuonana nae, tofauti na alivyokuzoe na kukusifia kwamba wewe ni mzuri sana, mrembo sana nk.siku hiyo tengeneza Mkorogo fake aidha kwa kuchukua poda na kuichanganya na mafuta kisha pakaa bila mpangilio mzuri na ondoka kwa ajili ya kwenda kuonana nae. 


Najua ukifika atakuuliza umekuwaje usoni mbona hivyo? Wewe mwambi umeunguzwa na Mkorogo na hujui cha kufanya maana umetumia kila dawa bila mafanikio.


Baada ya hapo kuwa makini kuanza kupokea majibu, kama hatakuambia "Ok! pole sana huku ananyanyuka kwenye kiti na kujifanya anaongea na simu huku akiondoka basi tarajia lolote hapo.


Lakini ukiona amesikitishwa na hiyo hali yako na kuahidi kukusaidia japo kwa ushauri nini cha kufanya basi jua huyo ana mapenzi ya kweli kwako na itakupasa kuanzia hapo ushikirie sana, Maana maplay boy huwa hawana la kusema zaidi ya kusepa.



No comments:

Powered by Blogger.