SEHEMU YA NNE: TARIME ZIPO MILA ZA KUKUMBATIA, LAKINI SI UKEKETAJI.
![]() |
Wasichana wakikeketwa |
Ukweli ni
kwamba elimu zaidi inahitajika kutolewa kwa wazee wa kimila, mangariba sanjari
na jamii nzima kwa ushirikiano wa karibu kabisa na serikali pamoja na wadau
mbalimbali yakiwemo mashirika na taasisi binafsi ili kuweza kuwaokoa wasichana
hawa kutoka katika janga hili la ukeketaji.
Jukumu la kupambana
na vitendo vya ukeketaji ni la jamii nzima, ambapo hapo kuna kundi kubwa la
waalimu ambalo lina nafasi mhimu katika kutoa elimu wa watoto wa kike juu ya
kupinga suala hili kama ilivyopendekezwa na Mwalimu Irene Massau kutoka shule
ya msingi Kibumaye alipokuwa akizungumza na mwandishi wa makala hii.
“Tunaomba
serikali iweze kutumia asasi za watu binafsi ili waweze kutoa elimu kwa walimu;
ili walimu nao waanze kutoa elimu kwa wanafunzi ili waweze kujua madhara ya
ukeketaji; kwa sababu wakishakeketwa huwa wengi wao unakuta wanapata mimba za
utotoni; unakuta mototo ana miaka 15
anaolewa na matokeo yake anapata mimba ambapo matokeo ya mimba za utotoni
yanasababisha vifo” alisema mwalimu Massau.
Mpenzi
msomaji matarajio yangu ni kwamba utakuwa wa kwanza kuchukua hatua ya kuokoa
japo kwa kutoa taarifa katika vyombo vya dola ama taasisi zilizo mstari wa
mbele katika kupigania haki za watoto wa kike katika kutokomeza kitendo hiki
katili cha ukeketaji.
Lakini kabla
sijahitimisha labda nikueleze tu kwamba katika makala hii nimeamua kujikita tu
katika Mila ya ukeketaji ambayo imekuwa mwiba mkali kwa watoto wa kike katika Wilaya ya Tarime, lakini
kama ulikuwa na kiu ya kuzifahamu baadhi ya mila na desturi ambazo ni mhimu
kuenziwa katika Wilaya hiyo basi ni pamoja na Mila ya Kuzindika.
Mila hii
hutekelezwa katika kipindi maalumu kama vile kipindi cha njaa ama vita ambapo
mnyama huchinjwa na watu hula sanjari na kunywa pombe ya asili kama vile machicha kwa lengo la kuondoa majanga (nuksi) kama hayo (njaa ama vita nk) katika jamii.
MTANZANIA MEDIA: Kusoma Makala hii kuanzia mwanzo hadi Mwisho bonyeza MAKALA utasoma kuanzia seheme ya kwanza hadi ya nne. Maoni na Ushauri 0757 43 26 94.
No comments: