TAFAKARI NZITO KABISA JUU YA NAMNA YA KUKABILIANA NA MAMBO MAGUMU KATIKA MAISHA YAKO.
Mwandishi wa Makala hii John Gabriel anasema kuwa Kuna
maswali mawili ambayo karibu kila siku anaulizwa hukO nchini Colombia. Miongoni mwa maswali hayo ni
"hivi kiswahili kipoje? embu zungumza maneno kadhaa ya Kiswahili tusikie
mnavyoongea".
Na swali la pili : " Je, umewezaje kujifunza kihispaniola kwa muda mfupi hivyo (Miezi 5) na sasa unasoma degree kwa lugha hii (Hatutumii English, ni spanish mwanzo mwisho), je sio ngumu kweli ?"
Tafakari yetu ya leo inahusu hili swali la PILI. Je, sio ngumu kweli kujifunza lugha ngeni,tena ndani ya muda mfupi hivyo ?
Jibu la swali hili ni kuwa watu hawafanyi mambo makubwa eti kwa sababu ni rahisi kwao kufanya hivyo, bali ni kuwa wamekubali kuwa ni magumu, ila wanajua pia kuwa wanahitaji kushinda ugumu huo, NA LA MSINGI ZAIDI NI KUWA WANAAMINI WANAWEZA KUUSHINDA UGUMU HUO.
Elewa katika kufanikisha mambo haitoshi tuu kujua kuwa suluhisho la ugumu lipo, bali wewe mwenyewe unayekabiliana na ugumu ujue kuwa UNAWEZA KUPITA SALAMA na KUSHINDA UGUMU HUO.
Unaweza kusoma kila siku tafakari za Mbuke Times, zikakupa hamasa kweli kweli, unaweza soma Inspirational Quotes hata 100 kwa siku, unaweza soma vitabu na kusikiliza au kuangalia makala za mbinu za ujasiriamali, kupata mafanikio na jinsi ya kubadili tabia, ILA kama wewe mwenyewe hauamini unaweza kufanya MABADILIKO, basi ni kazi bure.
Ukiamini utaweza kukabiliana na changamoto utakazokutana nazo. Kumbuka UNAWEZA CHOCHOTE Ukiamini UNAWEZA na UKATIA JUHUDI.

No comments: