SABABU SITA AMBAZO WATU WANAOTAKA MAFANIKIO HUWA NAZO.
Siri ya mafanikio mara nyingi huwa inategemea namna unavyojijengea mkabala wa mafanikio katika maisha yako. Kuna nadharia nyingi au kanuni za kwa namna gani binadamu anaweza kupata kile anachokihitaji maishani.Pamoja na nadharia hizo na mikabala hiyo pia zipo sababu ambazo watu wanaotaka mafanikio huwa nazo, sababu hizo ni kama ifuatavyo:-
1.
UBINAFSI, hii ni tabia inayomwezesha mtu kufanya maamuzi yanayozingatia matokeo
ayatakayo. Na sio ile tabia ya kitoto unayoijua wewe ya changu ni changu siyo
hiyo. Ubinafsi unaozungumzwa hapa ni wa kulenga au kuhitaji matokeo fulani
unayoyataka. Unapokuwa mbinafsi unakuwa na tabia ya kuuliza namna ya kutumia
muda, nishati na pesa ili vitu hivyo vikusogeze katika lengo. Ni vigumu kuwa
mbinafsi pasipo kujua aina ya maisha unayotaka kuishi.
Kitu unachotakiwa kujifunza ni kuchagua aina ya maisha unayotaka kuishi
na unapojifunza kuchagua aina ya maisha unayotaka kuishi ndio hivyo unakuwa
mbinafsi. Watu wengi sana sio wabinafsi kwa sababu hawana uchaguzi mzuri wa
maisha , matokeo yake wanakuwa ni watu wa matatizo siku zote. Kwa mfano takwimu
zinaonyesha kati ya watu 100 ni watu watatu au wanne tu ambao ni wabinafsi
nikiwa na maana kwamba hawa ndio wenye uchaguzi halisi ikiwa ni pamoja na
kupanga malengo na kuyatimiza.
2.NGUVU
YA MWELEKEO. Ni ngumu sana kuwa na nguvu ya mwelekeo kama
hujui unakoelekea. Bila mitazamo makini huwezi kuwa na nguvu ya mwelekeo kwenye
matokeo unayo yahitaji. Ni rahisi sana kupumbazwa, kukosa mpangilio na kupoteza
msimamo. Nguvu ya mwelekeo (Nguvu ya uzingativu) zinakuwa na madhara makubwa
sana na ya faida katika kukufanikisha. Na ninaposema nguvu ya mwelekeo kama
bado hujanielewa vizuri ni nguvu ya kushikilia kitu kimoja au kung’ang’ania
lengo moja mpaka uone matokeo.
3.
NIDHAMU, kama umeamua kuzifikia ndoto zako lazima uwe na kitu kinachoitwa
nidhamu, hii ni tabia ya kufundishwa pia inatokana na udhibiti binafsi. Kuwa na
nidhamu maanake ni kwamba hutayaacha malengo yako, kwa vile unajenga maisha
unayoyataka, basi nidhamu ni zana muhimu sana.
Nidhamu inakufundisha kuwa maisha sio tambarare, yana miinuko na
uzoefu unakufundisha kuwa ukiwa na maisha ya nidhamu unaweza kupita kwenye
miinuko hiyo.
4.UNG’ANG’ANIZI, ni hali
ya kuendelea na matokeo fulani bila kukata tamaa. Malengo yako yanafahamika,una
dira, una nidhamu na ni mbinafsi lakini unakutana na vikwazo. Haja tu ya kutaka
kuendelea hukufanya uvione vikwazo hivi kama nafasi badala ya tatizo.
Hata hivyo kama ingekuwa rahisi, basi kila mtu angefikia hapo
ulipo, lakini si kila mtu yupo kwenye
uwanja wa vita pamoja nawe. Wengi sana huwa wanasimama pindi wakutanapo na
vikwazo. Wewe unaona vikwazo na kuona nafasi papo hapo. Unajua unakoenda na
unajua huwezi kuzuiliwa na kitu chochote. Ung’ang’anizi wako ndio unaokuvuta
mbele. Unatafuta njia penye kizuizi chochote.
5.
UMILIKI, hii ni hali ya mmiliki. Ni kuchukua haki ya kumiliki kitu. Hapa ni ndoto
zako,malengo na maisha yako. Usipochukua jukumu la kuzimililki ndoto zako
mwenyewe, ni nani atafanya hivyo? Jifunze kumiliki ndoto zako na utaona matokeo
yake kwani kila ukitendacho kitafanikiwa na utapata matokeo uyatakayo.
Mara nyingi huwa tunatumaini mema wakati unapanga kwa mabaya. Kweli
uko tayari kwa chochote unachopewa na haya maisha? Unapochukua umiliki ni
kufanya mabadiliko ya kukusaidia kukupeleka mbele, kubadili tabia zisizo na
tija, labda hata kubadili marafiki wasioeleweka, kushugulika na dunia kadri
ilivyo na sivyo wewe unavyotaka iwe.
6.KUPIMA
MATOKEO, Siyo jambo dogo matokeo yanatakiwa kuwepo katika hali fulani ambayo
wewe mwenyewe umepanga. Uliweka malengo na matokeo uyatakayo, ulipanga
unavyotaka mambo yaishie na kwa vile unaumiliki, nguvu ya mwelekeo, na nidhamu
na fahamu kuwa una mbinu, msukumo,tama na uelewa na tayari una ramani
inayokuelekeza pa kwenda. Matokeo na kupima ni njia ya mafanikio. Hakuna
visingizio,hakuna kujuta, ni matokeo tu,hakuna kujaribu bali kufanya tu. Mambo
yanapoharibika hakuna kusononeka ni kuwajibika tu ndiko kunakotakiwa.
Kwa kifupi hizi Ni baadhi ya sababu ambazo watu wanaotaka mafanikio
huwa nazo na wewe pia unaweza ukajifunza na kusonga mbele zaidi ya ulipo,
nakutakia kila la Kheri katika safari ya maisha.
KWA HISANI YA AMKA MTANZANIA
No comments: