LIVE STREAM ADS

Header Ads

JIJI LA MWANZA KUTETEA UBINGWA WAKE KWA MARA YA TISA MFULULIZO?


Mzunguko wa Samaki Jijini Mwanza

 Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Halifa Hida amebainisha kwamba, Halimashauri ya Jiji la Mwanza inatarajia kuwa mwenyeji wa Maadhimisho ya Siku ya Usafi na Mazingira Kitaifa, yanayotarajiwa kuadhimishwa  June Tano Mwaka huu.

Akitoa Taarifa hiyo Wiki hii mbele ya Baraza la Halimashauri ya Jiji la Mwanza wiki iliyopita, Hida ameeleza kuwa Maandalizi ya Siku hiyo yamekwisha anza, ambapo amewataka viongozi mbalimbali wa Serikali za Mitaa kuhakikisha Mitaa yote ya Halimashauri ya Jiji inakuwa katika hali ya Usafi.

Ameongeza kuwa kwa mara ya Tisa Mwaka huu, Halimashauri ya Jiji la Mwanza inafanya kila juhudi ili kuhakikisha kwamba inatetembea Ubingwa wake wa kuwa Jiji Safi hapa nchini, Ubingwa ambao Halimashauri hiyo imekuwa ikiushikilia tangu kuanzishwa kwa mashindano ya Majiji Safi hapa nchini Mwaka 2006.

Aidha amewataka wananchi kuhakikisha kuwa wanaweka Mitaa yao katika hali ya Usafi katika kipindi hiki cha kuelekea katika Maadhimisho hayo, kwa kuwa Jiji la Mwanza litapokea wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi ambao watazunguka katika Mitaa mbalimbali ya Jiji kujionea hali ya Usafi wa Mazingira na Mitaa ya Jiji la Mwanza.
                                        
JE JIJI LA MWANZA LINASTAHILI KUTETEA NAFASI YAKE YA JIJI SAFI HAPA NCHINI MWAKA HUU KWA MARA YA TISA MFULULIZO? JE SERA YA KUFANYA USAFI KILA JUMAMOSI YA MWANZO WA MWEZI JIJINI MWANZA IMEZAA MATUNDA? PIA KWA NINI MAENEO MENGI HAPA NCHINI YAKIWA YANAPOKEA WAGENI NDIO MKAZO WA USAFI UNAHIMIZWA?

No comments:

Powered by Blogger.