LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHULE YA MSINGI NYANZA ILIYOKO JIJINI MWANZA, KUADHIMISHA JUBILEE YA MIAKA 83 MWAKA HUU TANGU KUANZISHWA KWAKE.

Katika kuadhimisha Jubilee ya Miaka 83 tangu kuanzishwa kwa Shule ya Msingi Nyanza iliyoko Mkoani Mwanza, wanafunzi waliowahi kusoma katika shule hiyo wameandaa mkakati wa kuhakikisha kwamba wanaifanyia shule hiyo Ukarabati.

Mbali na kuifanyia shule hiyo ukarabati kutokana na baadhi ya majengo yake kuwepo kwa muda mrefu tangu shule hiyo kuanzishwa mwaka 1931, wanafunzi hao pia wamepanga kuisaidia shule hiyo katika kupata zana za kujifunzia ikiwemo Komputa.

Ili kufanikisha Mpango huo, wiki chache zilizopita
wanafunzi hao ambao wamewahi kusoma ama kuhitimu katika shule hiyo ya Msingi ya Nyanza, wameunda kamati ambayo itahakikisha kwamba mipango yote ikiwemo ya upatikanaji wa fedha inakamilika mapema mwaka huu wakati shule hiyo inatimiza Miaka 83 tangu kuanzishwa kwake.

Viongozi waliochaguliwa ili kuisimamia kamati hiyo ni pamoja na Dkt.Emmanuel Chacha ambae alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, akisaidiana na Husein Kubah ambae alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo.

Akizungumza katika hafla ya chakula cha jioni kwa wanafunzi waliosoma Nyanza iliyofanyika katika Hotel ya JB Belmont jana usiku, Mwalimu Ulinyelusya Tumbo ambae ni Mkuu wa Shule hiyo aliechaguliwa pia kuwa Mhasibu wa kamati hiyo, amewasihi wanafunzi wote waliowahi kusoma ama kuhitimu katika shule hiyo kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha Sherehe hizo za Jubilee hiyo ya Miaka 83 ya Nyanza.

Katika chakula hicho cha Usiku ambacho kiliambatana na uundwaji wa kamati ya Kusimamia Jubilee hiyo ya Miaka 83 ya Nyanza, Jumla ya Shilingi Milioni Sita, laki Sita na Elfu arobaini ziliweza kupatikana kama mwanzo wa kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.

No comments:

Powered by Blogger.