LIVE STREAM ADS

Header Ads

DAH: MIAKA YAO YOTE, WAWILI HAWA WANAISHI BILA NYWELE NA MENO.

Unaweza Ukadhani ni kituko ama Kitu cha Kuchekesha, lakini Ukweli ni Kwamba, watoto wawili nchini Uganda, wameishi maisha yao yote mpaka hivi sasa,bila kuota Nywele wala Meno.

INNOCENT KYALIMPA Mwenye Umri wa Miaka 10, na AMBROSE  MUGISA mwenye Umri wa Miaka 12, hivi sasa ni Wanafunzi wa darasa la Tatu katika Shule ya Msingi Kitwara, na Ni wakazi wa kijiji cha Kampundu, Kilo Mita 15 Kutoka Mjini Kiryandongo, Uganda.

Watoto hao wanaishi na Bibi yao Ngoziwe, ambaye amekuwa nao tangia mama yao Mzazi alipowatelekeza, huku Wakikutana na Changamoto tofauti ikiwemo Kutengwa, Kutukanwa, pamoja na Kuathiriwa na Mionzi ya Jua.

Kwa mujibu wa Mtaalamu wa masuala ya Ngozi Nchini Uganda, Dk. FRED KAMBUGU, amesema kuwa tatizo hilo ni la Kurithi ambalo Kisayansi huitwa congenital ectodermal dysplasia (KONJENITO EKTODEMO DAISPLASIA), na husababisha Mtu kutokuota Nywele, Meno, Kucha na Mengineyo.

Watoto hao wawili hawana Uwezo wa Kula chakula Kigumu, huku wakijitahidi kukwepa Jua ili wasiumie.
Credit:New Vision & Black Touchez

No comments:

Powered by Blogger.