LIVE STREAM ADS

Header Ads

JAMAA AINGIA NA KENGE JIJINI MWANZA. AZUA BALAA KWA WANANCHI.

Jamaa mmoja amezua balaa Jijini Mwanza baada ya kufika katika eneo la Kamanga akiwa amemshikilia Kenge Mkononi, hali iliyosababisha watu wote waliokuwa katika eneo hilo kila mmoja kutimua mbilo pasi na kujua anakoelekea.

Jamaa huyo alikutwa na Mtanzania Media jana katika eneo la Kamanga nyuma ya Uwanja Mkongwe wa Nyamagana Jijini Mwanza akiwa na Kenge huyu Mtoto na haijahafamika alikomtoa. Jamaa alikuwa na Ujasiri sana maana alikuwa akimchezea Kenge huyu kama vile wamezaliwa wote pamoja.

Mtanzania Media iliondoka katika eneo hilo na kumuacha jamaa bado akiwa amemshikilia Kenge huyo na haifahamiki kilichojili baada ya hapo maana jamaa alikuwa ameanza kumtumia Kenge huyo kwa matumizi haramu ya kuwatishia watu ambao walikuwa wakipita katika eneo hilo la Kamanga nyuma ya Uwanja Mkongwe wa Nyamaga ambako inapita Reli inayoelekea eneo zinakopaki Ferry na Meli maarufu kama Kamanga Ferry.Tazama Picha.
Kenge aliekutwa eneo iliko Reli ya kuelekea Kamanga Ferry Nyuma ya Uwanja wa Nyamagana Mkoani mwanza.
Huyu akikutandika na Mkia wake naamini utajuta kuzaliwa.
Hapa ilikuwa baada ya kumchezea Kenge huyo kwa dakika kadhaa na kusababisha Kenge huyo kuchoka sana.
Kenge aliekutwa eneo iliko Reli ya kuelekea Kamanga Ferry Nyuma ya Uwanja wa Nyamagana Mkoani mwanza.
Sjui kamtoa wapi huyu Kenge...Sisi tumeshangaa kuona mtu amemshikilia Kenge Mkononi bila hata woga wowote.
Mwanangu Mwenyewe huyu..Huyu ndie Jamaa aliekutwa na Kenge  na hapa alikuwa akimchukua Kenge wake.Mtanzania Media haina uhakika kama anammiliki kiuhalali ama laaah, Maana alikuwa mkali mara baada ya kugundua anapigwa picha hali iliyomlazimu mpiga picha wetu kutimua mbio baada ya kutishiwa kupigwa na huyu Kenge.Hakuna imani ya aina yoyote kuhusiana na Kenge huyu.

No comments:

Powered by Blogger.