LIVE STREAM ADS

Header Ads

MICHUANO YA SAFARI LAGER POOL TABLE MKOANI MWANZA KUANZA LEO.

Wa kwanza (kushoto) ni Michael Gioche ambae ni Mwakilishi kutoka club inayotetea Ubingwa wa Michuano ya Safari Lager Pool Table Mkoani Mwanza,Wa Pili ni Sweetbert Victor ambae ni katibu wa Pool Table Mkoani Mwanza (MZAPA), Watatu ni Kizito Sosho Bahati ambae ni Afisa Michezo Manispaa ya Ilemela na wa mwisgo (kulia) ni Mudi Bitegeko ambae ni Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi Mkoa wa Mwanza (MZAPORA).
Washiriki wa Michuano ya Safari Lager Pool Table Mkoa wa Mwanza kwa mwaka huu jana wamekabidhiwa jezi kwa ajili ya Michuano hiyo ambayo inafanyika asubuhi ya leo.Michuano hiyo inafanyikia Shooters Pub iliyoko Kirumba Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Kizito Sosho Bahati (wa kwanza Kulia) akimkabidhi jezi mwakilishi kutoka club ambayo ni bingwa mtetezi wa Michuano ya Safari Lager Pool Table Mkoani Mwanza.Bingwa Mtetezi wa Michuano hiyo ni PS Club Kutoka Pasinasi.
Washiriki wa Michuano ya Safari Lager Pool Table mwaka 2014 Mkoani Mwanza wakikabidhiwa jezi kwa ajili ya michuano hiyo ambayo inafanyika asubuhi ya leo Shooters Pub.
Baadhi ya Washiriki wa Michuano ya Safari Lager Pool Table Mkoa wa Mwanza inafanyika mapema asubuhi ya leo ambayo inafanyika Shooters Pub ikiwa inashirikisha jumla ya Vilabu 8. Vilabu vinavyoshiriki Mashindano hayo ni pamoja na Bingwa Mtetezi PS Club kutoka Pasiansi, Beach Boy, OMAPA Pool Club, Wanyama Pool Club, Kitwine Pool Club, Golden Club na Gilliard Pool Club.

No comments:

Powered by Blogger.