KOMBE LA DUNIA: OIRIGI NI NOMA, AISAIDIA UBELJIJI KUSONGA MBELE.
Divock Origi aifungia Ubeljiji bao la Ushindi.
Tineja aliyezaliwa Kenya na
kuchukua uraiya wa Ubeiljiji Divock Origi alifungia Ubeljiji bao la
pekee na la ushindi dhidi ya Urusi katika mechi yao ya pili ya kundi H. Bao hilo la dakika za mejeruhi za mechi hiyo ndiyo iliyoiwezesha Ubeljiji kufuzu kwa mkondo wa pili wa timu kumi na sita bora.
Awali Ubeljiji ilikuwa imemjaribu Igor Akinfeev ila mkwaju wake Kevin Mirallas ukagonga mwamba.
Ushindi huo uliiwacha Ubeljiji kileleni mwa kundi hilo wakiwa na alama 6 baada ya ushindi wao wa pili.
Wenyeji wa mashindano yajayo ya kombe la dunia mwaka 2018 Urusi watalazimika kufanya kazi ya ziada ilikufuzu kufuatia matokeo mawili ya kwanza huko Brazil
Lukaku; Ubeljiji 1-0 Urusi
Hata hivyo Kocha Fabio Capello amesalia na mechi dhidi ya Algeria kujaribu bahati yake na mfumo mpya kabla ya kuabiri ndege ya Moscow.
Nchini Kenya ambapo Origi alikuza talanta yake ,wakenya wamemmiminia sifa kochokocho tineja huyo ambaye babake aliwahi kuichezea Harambee Stars .
Evelyn Wambui kwenye tweeter alisema kuwa #Origi anaiwakilisha kenya katika kombe la dunia #TeamKenya in the #Worldcup2014 !
@kevojuice naye aliandika kuwa Origi ndiye mchezaji wa kwanza wa kenya kucheza kwenye kombe la dunia '' 1st Kenyan to score in World Cup...!!! #Origi hehe...
Na bbcswahili.
No comments: