KOMBE LA DUNIA: URENO TAABANI BAADA YA SARE NA USA.
Bao la kusawazisha la Silvestre Varela
Ureno ambayo ilikuwa imepata
pigo kubwa iliposhiindwa katika mechi yake ya ufunguzi na Ujerumani na
ilikuja katika mechi hii ikitafuta ushindi wa aina yeyote ilikuepuka
fedheha ya kufungashwa virago katika hatua ya makundi katika kombe la
dunia linaloendelea huko Brazil.
Ureno imejipata taabani baada ya kutoka sare ya 2 -2 na Marekani
Marekani ilifufua matumaini ya kusonga mbele Clint Dempsey alipovurumisha mkwaju ndani ya neti na kuiweka timu yake mbele , hata hivyo Christiano Ronaldo alimwandalia pasi nzuri na akaisawazishia Ureno katika muda wa ziada wa mechi hiyo.
Ureno imejipata taabani baada ya kutoka sare ya 2 -2 na Marekani
Marekani inahitaji ushindi mkubwa dhidi ya Ujerumani ambayo itakuwa ikitafuta sare ya aina yeyote ilikusonga mbele.
Ghana kwa upande wao sasa wanahitaji kuichapa Ureno na kuomba kuwa Ujerumani nayo itaitandika Marekani iliwafuzu kwa mkondo ujao. Kufikia sasa ujerumai inaongoza kundi hili ikiwa na jumla ya ponti 4 sawa na Marekani.Ghana ni ya 3 na alama 1 sawa na Ureno.
Na bbcswahili.
No comments: