MICHEZO: MADAI YA UFISADI KATIKA SOKA YAIBUKA.
Kikosi cha soka cha Ghana
Shirikisho la soka nchini Ghana
limewataka maafisa wa polisi kuingilia kati baada ya madai ya vyombo vya
habari vya Uingereza kwamba mmoja wa maafisa wake alikubali timu ya
nchi hiyo kucheza katika mechi zilizo fanyiwa ufisadi.
Katika taarifa yake shirikisho la soka duniani FIFA limesema kuwa hakuna ushahidi kwamba uadilifu wa michuano ya kombe la dunia umeathirika. Shirikisho la soka nchini Ghana limesema kuwa litamuekea vikwazo vikali afisa yeyote atakayepatikana na makosa hayo.
Na bbcswahili.
No comments: