LIVE STREAM ADS

Header Ads

MINATO MIKALI: MC DARADA AFICHUA SIRI YAKE YA MIAKA MINGI.

Anafahamika kama Damian Raphael Damian aka MC Darada mzee wa Kikombe ambayo ni ngoma ilimtambulisha vyema katika game ya Bongo akiwa amefanya msanii mwenzi anaefahamika kama Dogo Poteza chini ya Mkono wa King Fenya ndani ya Studio za Mbunda Jijini Mwanza. Akizungumza na Mtanzania Media muda mfupi baada ya Kumaliza show ndani ya 99.4 Metro FM Kupitia kipindi cha Saturdaya Club Mixing Jumamosi Usiku, Mc Darada alisema kuwa yeye ndie Msanii pekee kutoka Jijini Mwanza ambae anajua kuuvalisha mwili wake pamba kali pengine kuliko Msanii yeyote kutoka Jijini Mwanza.
"Unajua braza kiukweli mimi najikubali sana kwa kutupia pamba kali...simemi kwamba wasanii wenzangu wanaotokea Mwanza ama walioko Mwanza kwamba hawajui kutupia pamba kali, lakini Ukweli ni kwamba hawafikii level zangu....Na naongea hivi kiroho safi kabisa wala asije akatokea msanii wa Mwanza akanielewa vibaya maana ni jambo la kawaida mtu kueleza ukweli ulio ndani ya moyo wake....na napenda nikuibie siri kwamba hata mashabiki zangu hili huwa wanalijua...wanajua kuwa Darada kwa pamba kali anatisha na naomba GB ufahamu kuwa hii ni siri ambayo nimekaa nayo kwa muda mrefu sana hivyo ni wakati sasa mafans wangu kujua kuwa mimi mzee wa pamba kali na nafanya hivyo kwa ajili yao maana wengi hupendezwa na uvaaji wangu" Alisema Mc Darada.
Mbali na Ngoma ya Kikombe Mc.Darada pia ana ngoma kibao ikiwa ni pamoja na Bora ungesema, Usiniache, Demu Noma, Mama wa Kambo huku tayari akiwa na ngoma Mpiya ambayo soon ataiachia, ni ngoma ambayo inafahamika kama Ngololo. Ngoma hii imetengenezwa ndani ya studio za Mbunda ikiwa ni mkono wake King Fenya the Beat. Ngoma hii iko tayari kinachosubiriwa ni Video yake ili kwa Audio na Video zitoke kwa pamoja.
Kama hujawahi kusikia ngoma japo hata moja ama kutizama video zake, basi ingia Youtube na andika Mc.Darada utapata video zake na utacheki namna jamaa alivyo mnomaaaa.
"Unajua Braza GB Mwanza kuna wasanii wakali sana sema tu hawajui na ndiyo maana wanajikuta wakianza kupata jina kidogo tu wanakimbilia Mikoa Mingine kama Dar kitu ambacho mimi sikuungi Mkono. Dara nitakwenda kwa ajili ya kazi kama nimeitwa lakini siyo kuhamishia shughuli zangu zote za mziki huko, hata huku huku Mwanza tunaweza kufanya mziki na tukaeleweka na tukawa tunaenda Mikoa mingine kupiga show na kurudi kama wanavyofanya wasanii walioko Dar, kwamba wanaenda Mikoani wanapiga showz na wanarudi Dar" Alisema Mc.Darada huku akiongeza kuwa kwa yeyote anaehitaji kufanya nae kazi basi amchecki kwa namba hii hapa 0766 93 26 35 kwa mawasiliano zaidi.

No comments:

Powered by Blogger.