MUIGIZAJI MKONGWE HAPA NCHINI MZEE SMALL AMEWAHI KUZUSHIWA KIFO MARA KADHAA...SOMA HABARI HII YA KUSIKITISHA JUU YAKE.
Mtoto wa marehemu
aitwaye, Mahmud (Mongamba) amethibitisha kifo cha Mzee Small ambapo ameeleza kuwa siku ya jana alishinda nae ila ilivyofika saa nne usiku kafariki akiwa mikononi mwake.
Aidha amebainisha kuwa baba yake alipelekwa Hospitalini Mhimbili jana Jumamosi tarehe saba majira ya saa mbili za asubuhi baada ya kuzidiwa.
Mara kadhaa Mzee Small amewahi kuzushiwa kifo na kupelekea taharuki kuwa kwa mashabiki zake, lakini mara hii si uzushi tena na ni habari za kweli kuwa Mzee Small hatunae tena na hivyo kufanya habari ya kifo chake ambayo mara kadhaa iliwahi kugeuka kuwachekesha wapenzi wake baada ya kugundua yu hai, tofauti na hii ya sasa ambayo imegeuka kuwa simanzi huku wengine wakidhania ni utani kama wa awali na kuhisi labda ataamka tena, lakini ni kweli Mzee Small hatunae tena.
Mungu ailaze Roho yake Mahala pema peponi, amen!
No comments: