 |
Nahodha
wa Klabu ya Billiard, Becka Mbulla (kulia) akitoa fedha taslimu
Shilingi 800,000/= kwenye bahasha mara baada ya kukabidhiwa na
Mwakilishi wa Kampuni ya Bia nchini (TBL), Bernard Issaria (kushoto)
mara baada ya kuibu bingwa katika mashindano ya Pool Mkoa wa Mwanza
yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014” yaliyo
malizika mwishoni mwa wiki mkoani humo. Katikati ni Katibu wa chama cha
Pool Mkoani humo, Switbart Victor.
Klabu ya Billiard ya Mwanza, New
Stand
ya Shinyanga na Yakwetu Pwani zimefanikiwa kutwaa ubingwa wa mikoa katika fainali za mashindano ya mchezo wa
Pool ngazi ya Mikoa yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014” yaliyo malizika mwishoni mwa
wiki mikoani humo na kuzawadiwa kila klabu fedha taslimu Shilingi 800,000/=
pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa kwenye fainali za Kitaifa zinazotarajiwa kufanyika Mkoani
Kilimanjaro.
Billiard ya Mwanza ailitwaa ubingwa kwa kuifunga Klabu ya Wanyama
13-11, New Stand ya Shinyanga ilitwaa ubingwa kwa kuifunga klabu ya The Ganner 13-7
na Yakwetu ya Mkoa wa Pwani ilitwaa ubingwa kwa kuifunga klabu ya Kiluvya 13-12.
|
 |
Nahodha
wa Klabu ya Billiard, Becka Mbulla (katikati) akihesabu fedha taslimu
Shilingi 800,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya
Pool Mkoa wa Mwanza yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition
2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki.
Upande wa mchezaji
mmoja mmoja wanaume Mwanza, Lameck Omary (Ndala Ndefu) alifanikiwa
kutwaa ubingwa wa mkoa na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi
400,000/= kwa kumfunga Hans Fabian 5-2 ambapo Hans Fabian
alizawadiwa fedha taslimu Shilingi 250,000/=.Mkoani Shinyanga, Paul
Filaki alifanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa na kuzawadiwa fedha taslimu
Shilingi
400,000/= kwa kumfunga Fredrick Njele3-0ambapo Fredrick
Njele alizawadiwa fedha taslimu Shilingi
250,000/=.na Mkoa wa Pwani, Anold Djofu alifanikiwa kutwaa ubingwa wa
Mkoa huo na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi
400,000/= kwa kumfunga Michael Njau 3-2
na hivyo Michael Njau alizawadiwa fedha taslimu Shilingi 250,000/=.
|
 |
Nahodha
wa Klabu ya Billiard, Becka Mbulla (katikati) akihesabu fedha taslimu
Shilingi 800,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya
Pool Mkoa wa Mwanza yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition
2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki mkoani humo. |
Mchezaji mmojammoja Wanawake waliofanikiwa kutwaa ubingwani,
Mwanza-Rukia Issa, Shinyanga - Sada Tullah na Pwani ni Fatma Kihongo ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi
300,000/=
kila mmoja pamoja na tiketi ya kuwakilisha mikoa yao katika fainali za Kitaifa Mkoani
Kilimanjaro.
Fainali za kitaifa za
2014 za “Safari National Pool Competion” zinatarajiwa kufanyika Moshi Mkoani
Kilimanjaro kwa kushilikisha Mikoa 17 ambayo ni Tabora, Shinyanga, Dodoma
Mbeya, Iringa, Morogoro, Mwanza, Kagera, Manyara, Arusha, Tanga, Pwani, Ilala, Lindi, Temeke, Kinondoni
na wenyeji wa mashindano kwa mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro.
No comments: