LIVE STREAM ADS

Header Ads

NDOA ZA WABUNGE NCHINI TANZANIA NI MATUSI TUPU KWA WAPIGA KURA WAO. SOMA KILICHOANDIKWA BAADA YA NDOA YA MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI MH.JOSHUA NASSARI.

Huu ni Mtizamo wa Tadei Ole Mushi aliyouwasilisha kupitia ukurasa wake wa facebook akiangazia ndoa ya Mbunge wa Arumeru Mashariki aliefunga ndoa juzi jumamosi na bi.Anande Nnko.

Safari ya kuuondoa umaskini TANZANIA unahitaji weledi wa hali ya juu tofauti kabisa na wenzetu wa KENYA. Viongozi wetu wanapenda sana starehe kuliko kazi tofauti na wenzetu wa KENYA.
Jana (jumamosi) mbunge Nasari ametumia milioni 96 kufanikisha harusi yake wakati upande wa pili mbunge mwingine kijana toka Kenya Carol Nkirote yeye kafanya sherehe ya kawaida kabisa bila mbwembwe za kubebwa bebwa unaambiwa haizidi milioni 30 za kitanzania Carol Nkirote alizotumia.

Arumeru kuna matatizo mengi sana ambayo yangeweza kutatuliwa na hizi fedha angefanya sherehe ya kawaida halafu fedha nyingine ikasaidia wananchi au akaificha kwenye account yake kuliko kuwaonyesha wananchi wa meru tambo hizi.

Juzi juzi tu Vicky Kamata alikuwa afanye kufuru ya milioni Mia moja kabla ya ndoa kuyeyuka nafikiri hizi fedha azielekeze jimboni kwake wananchi wapate maji safi ya kutumia.

No comments:

Powered by Blogger.