PAMOJA NA UBORA WA KAZI ZA DIAMOND PLATNUM, HII NI SABABU NYINGINE INAYOMFANYA AKUBARIKE KATIKA JAMII.
Macho
na masikio ya Watanzania wengi kwa siku ya Jumamosi June 07 yote
yalielekezwa Durban Afrika Kusini sehemu ambako zilikua zikitolewa tuzo
za wateule wa MTV Afrika Music Award ‘MAMA’.
Furaha tuliyokuwa nayo Watanzania ilikua kubwa baada ya kuona kijana
kutoka nyumbani Tanzania kuwa ni miongoni mwa vijana wanaochuana kwenye
tuzo hizo tena akiwa vipengele viwili,ingawa bahati haikua njema kwa
Diamond kwani hakufanikiwa kupata tuzo alizokuwa akiwania, ambazo ni mwanamziki bora wa kiume na ile ya wimbo bora wa kushirikiana.Baada ya kutangazwa washindi hao na yeye kutokuwepo Dimand Platnumz ameandika maneno haya kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii;
’Maisha ni Hatua.. Nafikiri kwa mwaka huu ile ndio ilikuwa hatua yetu kwa MTV…Cha muhimu ni kujua wapi tulipokua mwaka jana na wapi tulipo leo… pia kujifunza na kujua ni nini cha kuongeza zaidi ili Next tym tuzidi kufanya vyema…. Shukrani zangu nyingi ziende kwa Mashabiki wote,Management, Media,Family, wasanii na wadau Mbalimbali kwani kwa nguvu zao ndio zimefanya leo kunisogeza toka sehem moja kwenda nyingine…Next stop #BET!!!… Asante sana #Sheriangoi kwa Suti Hii’.
Kushukuru ndio jadi yetu, Diamond ametambua umuhimu wa wadau na watu mbalimbali ambao wanamfanya akubarike, hivyo ameamua kutoa shukurani zake jambo ambalo linaonyesha mapenzi aliyonayo kwa watu wake, hakika hiki ndicho kinachomfanya Diamond akubarike katika jamii, wasanii wengine igeni mfano huo na kuondokana na nyodo na mapozi yasiyo na maana kwa waliowafanya mfanikiwe katika sanaa.
Diamond Platnumz alikuwa pia ni moja kati ya watumbuizaji wa ugawaji wa tuzo hizi,ambapo kwa namna alivyoingia kwenye jukwaa na Davido ilimfurahisha kila mtu aliyekuepo ukumbini na watu waliokuwa wakiangalia nyumbani kupitia DSTV.
Kwa Ushirikiano na MillardAyo
No comments: