RAIS WA CHUO KIKUU BUGANDO NA MWENYEKITI WA VYUO VIKUU TANZANIA APATIKANA AKIWA HAJITAMBUI BAADA YA KUPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA.
![]() |
Pichani ni Mdede kabla hajatekwa |
Akiongea na mwandishi wa habari hii,waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi Bugando Benjamini Thomas,alisema Mdede aliletwa na vijana watatu,wanaume wawili na mwanamke mmoja waliodai kumuokota bwana Mdede katika eneo la Usagala akiwa hajitambui wala kujielewa,
Anaendelea kusema kwa mujibu wa mama
mwenye Nyumba wa Mdede,watu hao walidai baada ya kumuokota jana usiku
katika eneo hilo la Usagala,waliamua kumchukua na kwenyda kumuhifadhi
katika eneo la Igoma, alipoanza kupata fahamu na kueleza anaishi wapi
ndipo wakamleta nyumbani kwake,huku watu hao wakidai walishindwa kumleta
jana na asubuhi kutokana na Mdede kutojitambua na kuwa katika hali ya
kupoteza kumbukumbu,hata hivyo mama mwenye nyumba anasema watu hao
hawakukaa sana wakaondoka bila kutoa maelezo zaidi.
Waziri mkuu huyo wa Bugando aliendelea kusema, "kwa mujibu wa mama mwenye nyumba,alisema kwamba mara baada ya watu hao kumleta nyumbani hapo wakiwa wamempakia kwenye gari aina ya Kenta,walitoa maelezo machache na hawakutaka kukaa sana wakaaga wakaondoka ".
Kwa
mujibu wa waziri mkuu Thomas anasema kaka yake alijaribu kuwapigia mara
kadhaa lakini yeye hakupokea simu yake kwakuwa alikuwa anatoa tamko kwa
waandishi wa habari juu ya kupotea kwa Mdede,na walipomaliza kutoa
tamko walielekea kwa Mdede baada ya kuambiwa na kaka yake kila kitu,"na
tulimkuta anamwonekano, anahali dhoofu,akiwa anaongea kwa tabu na huku
akiwa hana kumbukumbu nzuri zaidi ya kumbukumbu ya kabla
hajatekwa"
Anaendelea kusema kuwa waliwasiliana na mkuu wa upelelezi wa wilaya
ya Nyamagana na wakakubaliana wasitoe taarifa kwanza mpaka watakapo
muhoji na kuangalia taratibu zingine za kiulinzi,na baadae ndipo
walipojiridhisha na kuamua kumpeleka hospitalini Bugando kwani awali
alikuwa akipatiwa matibabu palepale nyumbani kwake,lakini waliamua
kumpeleka hospitali hiyo kwa ajili ya vipimo na uchunguzi zaidi na hasa
walipoona hali ya Mdede haieleweki na wakahisi huenda akawa amelishwa
vitu vibaya kama sumu.
Na: Nicholaus Kilunga
No comments: