LIVE STREAM ADS

Header Ads

DIAMOND PLATNUM AMRUHUSU SWEET CAKE KUURUDIA WIMBO WAKE. ASEMA NAE ATASIKIKA PIA KWENYE HUO WIMBO.

Huyu ndie Msanii kutoka Jijini Mwanza ambae anafahamika kwa jina la Sweet Cake akiwa chini ya Producer Lol Pop ambae anasema kuwa Diamond Platnum amemruhusu kuirudia ngoama yake ya Nitarejea, ambayo ni ngoma iliyomuweka kwenye ramani ya Mziki mtu mzima Platinum. 

Anasema mara ya kwanza alikutana na Diamond Jijini Mwanza wakati Diamond akiwa na Show Buzuruga Plaza na alipopanda jukwaani kama msanii wa Mwanza aliimba ngoma ya Nitarejea ila kwa kuibadilisha na kuimba kama vile anatoa majibu ya ngoma ya  Diamond ya Nitarejea, yeye akaiita SI ULISEMA UTAREJEA.  
Akipiga story na Metro FM Sweer Cake alisema "Ilikuwa siku ya Show kule Buzuruga Plaza na nilipanda jukwaani na kuimba ngoma ya Diamond kwa kuirudia, na Platnum alipoisikia ilibidi apande jukwaani muda huo huo na kuniambia amekubali uimbaji wangu na akaniruhusu kuirudia hiyo ngoma ambapo pia aliniahidi kuweka mistari kweny hiyo ngoma. 
Tayari hiyo ngoma kwa vipande vya Sweet Cake vimekamilika hivyo anasubiriwa Platinum ili kuweka verses zake na mziko uweze kuachiwa.
Msanii Sweet Cake.
Mkali wa ngoma ya Uzuri wako ambae anafahamika kwa jina la Fresh B. Soon anatarajia kuachia ngoma mpya ikiwa na kichupa chake.Ngoma imesimamiwa na Lol Pop huku kichupa kikisimamiwa na One Love FX.
Msanii wa Hip Hop Kutoka Mwanza Young Liver ambae kwa sasa ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Ni Sisi Wenyewe, akiwa na vichwa kibao ikiwa ni pamoja na Mwanadada kutoka Dar Illumination.
Fresh kushoto, pale kati mwana dada Young Liver na Sweet Cake kulia ndani ya Studio za Metro FM Jijini Mwanza Usiku katika Show ya Saturday Club Mixing inayoruka kila Jumamosi kuanzia saa nne hadi saa saba Usiku na Mwanaharakati GB.Pazzo

No comments:

Powered by Blogger.