LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAARIFA KWA UMMA: NI KUTOKA KWA DK.TONNY AMBAE NI MTANGAZAJI WA RADIO METRO YA JIJINI MWANZA.

Dk.Tonny
Naombeni mniunge mkono kesho tarehe 12 eneo la viwanja vya posta kuanzia saa 3 asbh nitakwenda kuchangia damu,nitasindikizwa na wasikilizaji na futuhi,njoo tuchangie damu tuokoe maisha ya mama!

Huo ni Ujumbe kutoka kwa Mtangazaji wa Radio Metro FM ya Jijini Mwanza Alphonce Tonny Kapela maarufu kama Dk.Tonny ambao ameuandika Kupitia Ukurasa wake wa Facebook, akikusihi wewe Mkazi wa Jiji la Mwanza na Mikoa Jirani ambae una nafasi ya kuchangia damu na kuokoa maisha ya Watanzania (wahitaji wote) ambao wanauhitaji wa damu.

Iko hivi, kwa kutambua umuhimu na uhitaji wa damu hapa nchini, Dk.Tonny amejitokeza na kuratibu zoezi la kuchangia damu ambalo litafanyika siku ya kesho kuanzia majira ya saa tatu kamili za asubuhi katika eneo la Posta jirani na Uwanja wa mpira wa Nyamagana, ambapo zoezi hilo litafanyika ikiwa ni siku moja kabla ya siku ya uchangia wa damu kwa hiari ambayo itafanyika kesho kutwa june 14.

Katika zoezi hilo, Dk.Tonny atasindikizwa na wadau na wasikilizaji wa 99.4 Radio Metro FM, kundi la vichekesho la FUTUHI ambalo huonyesha vichekesho vyake kupitia Star TV sanjari na wadau wengine kama vile wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini ambapo zoezi hilo litapata baraka zote na Mpango wa Taifa wa Bank ya damu salama kanda ya Ziwa.

Meneja wa Posta Mkoa wa Mwanza Chief Chifungo anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika zoezi hilo, hivyo wakazi na wananchi wa Jiji la Mwanza na Maeneo ama Mikoa jirani mnakumbushwa kujitokeza kwa wingi katika kushiriki zoezi hili ambalo limelenga kupunguza upungufu mkubwa damu uliopo katika Bank ya damu ukilinganisha na uhitaji uliopo. 
 Mtanzania Media: Wengi hupoteza Maisha kwa kukosa damu, Jitokeze kuchangia damu ili uokoe Maisha ya watu wenye Uhitaji wa damu.


No comments:

Powered by Blogger.