LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAZAMA JINSI DK.TONNY KUTOKA RADIO METRO JIJINI MWANZA, ALIVYOOKOA MAISHA YA AKINA MAMA, WATOTO NA WOTE WENYE UHITAJI WA DAMU MKOANI MWANZA.

Anafahamika kama Mama Letty mpika Chapati Mahiri kutoka Nyakato Jijini Mwanza, ni mmoja kati ya wananchi waliojitokeza kuchangia damu katika zoezi ambalo limeratibiwa na Dk.Tonny ambae ni Mtangazaji wa Radio Metro ya Jijini Mwanza ikiwa ni siku moja katika kuelekea kwenye maadhimisho ya Siku ya Mchangia damu duniani itakayofanyika kesho
 
Mama Letty akihijiwa na Paulina David ambae ni Mwandishi wa habari kutoka Radio Free Afrika mara baada ya kujitokeza katika kuchangia damu hii leo. "Mimi nilivyosikia Dk.Tonny anatangaza radioni kuwa leo atakuwa anatoa damu na anahitaji watu wa kumuunga mkono, kiukweli niliguswa sana ikizingatiwa kwamba bado mahitaji ya damu hapa nchini ni makubwa hivyo nawasihi na wananchi wengine wawe na desturi ya kushiriki katika uchangiaji wa damu" Anasema mama Letty.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali pia walikuwepo ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kuihamasisha jamii kushiriki kadri iwezekanavyo katika kuchangia damu. Hapa naiona TV 1, Kwa Neema FM na Radio Free nk.
Dk.Tonny kutoka Radio Metro Fm ya Jijini Mwanza (Kulia) akiwa na Chief Chifungo (kushoto) ambae ni Meneja wa Posta Mkoa wa Mwanza ambae nae alikuwepo katika zoezi hili nzuri kabisa katika jamii, ambapo mbali na kushiriki katika zoezi hili pia ametoa ridhaa eneo la Posta kutumika kwa ajili ya kufanikisha shughuli hii, hakika anastahili pongezi.
Wadau wa Metro Fm, hakika mmeokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu.
Kesho ni Siku ya Mchangia damu duniani, Siku hii ilianzishwa mahususi kabisa kwa ajili ya Kutambua na kuenzi mchango wa Wachangia damu. Kitaifa maadhimisho ya Siku hii yatafanyika Mkoani Kigoma huku katika Mkoa wa Mwanza yakifanyika Igoma Wilayani Nyamagana.

k
"Dk.Tonny nami nimeona ni vyema nije nikuunge mkono katika shughuli hii ambayo leo umeifanya, hakika ww ni mfano wa kuigwa katika jamii, umeokoa maisha ya akina mama na watoto hivi tunavyozungumza..." Dk.Tonny kulia akiwa na Mdau wa Metro Fm kushoto wakibadilishana mawazo.

Wakati mwaka huu Taifa linaadhimisha maadhimisho haya, bado kuna changamoto ya upungufu wa damu katika hospital mbalimbali huku changamoto ya uuzwaji wa damu hiyo ikijitokeza katika baadhi ya hospital ambapo jambo hilo hufanywa na baadhi ya watumishi wasio na maadili licha ya kutambua kuwa ni kinyume cha sheria kumuuzia mgonjwa damu.

Vicent Muhada ambae ni Mhamasisha kutoka Mpango wa Taifa wa damu salama Kanda ya Ziwa anakiri kuwa bado kuna malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa wanauziwa damu, jambo ambalo linapeleka wananchi wengi kutojitokeza katika zoezi la uchangiaji wa damu kwa hiari.

Muhada akizungumza na Waandishi wa habari hii leo wakati wa zoezi la uchangia wa damu kwa hiari, zoezi ambalo limeratibiwa na Alphonce Tonny Kapela (Dk.Tonny) ambae ni Mtangazaji wa Radi Metro, ametoa rai kwa wananchi kuwa na desturi ya kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu kwa kuwa mado mahitaji ni mengi.

Aidha amewasihi wananchi kutoa taarifa pale wanapokumbana na vitendo vya kuuziwa damu.Amesema ni kinyumche cha sheria mgonjwa kuuziwa damu hivyo wananchi wanapokumbana na hali hiyo watoe taarifa kwa uongozi wa hospital husika, polisi, TAKUKURU ama katika uongozi wa Mpango wa Taifa wa damu salama, na hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mtumishi yeyote atakaebainika kujishughulisha na vitendo vya uuzaji wa damu.

Vicent Muhada (kulia) ambae ni Mhamasishaji kutoka Mpango wa Taifa wa damu salama Kutoka Kanda ya Ziwa akifurahi baada ya zoezi la kuchangia damu kuonyesha mafanikio makubwa.  Ilikuwa ni katika kupongezana na mtumishi mwenzie.

Dk.Tonny ndie alieongoza zoezi la kuchangia damu hii leo. Hakika ni mfano wa kuigwa katika jamii.Changia damu ili kuokoa maisha ya akina mama na watoto wadogo (wenye uhitaji wote pia)

Hii ilikuwa baada ya kumaliza kuchangia damu. "Kwa nini watu huwa hawana desturi ya kuchangia damu, mbona si zoezi gumu, nadhani elimu zaidi inahitajika kuendelea kutolewa ili kuongeza mwamko wa kuchangia damu..." Mmoja wa wachangiaji wa damu alisikika akisema mara baada ya kumaliza kuchangia damu.
Zaidi anafahamika kama Mika the Boy (kushoto) ambae ni mdau mkubwa wa Radio Metro na hapo alikuwa katika hatua za awali kwa ajili ya kuchangia damu. Safi sana wadau wa Radio Metro Jijini Mwanza kwa Kushow love na Dk.Tonny.
Kesho ndiyo Siku ya Maadhimisho ya Mchangia damu duniani.Soma kwa Makini Bango hilo. 







No comments:

Powered by Blogger.