LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAARIFA KAMILI KUHUSIANA NA MCHAWI ALIEDONDOKA KATIKA HOSPITAL YA MKOA WA MWANZA SEKOUR TOURE, NI BAADA YA KUGOMBANA NA WENZAKE WANNE AKIWEMO MAMA MCHUNGAJI.

Anaesadikiwa kuwa mtalaamu wa anga/mchawi.....(Picha Y.Kagenzi)
Mtu mmoja anaesadikiwa kuwa ni Mchawi ambae bado Mtanzania Media haijabahatika kupata majina yake kamili wala makazi yake, Usiku wa Kuamkia leo amedondoka kutoka angani karibu na viunga vya Hospital ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure zikiwa ni hatua chache kutoka zilipo ofisi za halmashauri ya jiji la Mwanza.

Duru za habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa mwanamke huyo alidondoka maeneo hayo baada ya kutokea kutokuelewana na wenzake wane aliokuwa nao, akiwemo mama mmoja ambae mwanamke huyo amemtaja kuwa ni Mama Mchungaji wa kanisa la...(Jina linahifadhiwa).

Mwanamke huyo amekutwa maeneo hayo akiwa na Taulo kiunoni ambapo katika kujitetea kwake amekiri kuwa yeye ni mchawi na amedondoka katika maeneo hayo baada ya kutokea ugomvi akiwa na wenzake ambao walimzidi nguvu na kumpelekea  yeye adondoke chini.

“Kwa maelezo niliyopewa alikamatwa (kitalaamu) wakati akienda kuwachukua watoto wadogo kwenye hospital hiyo (Sekour Toure) akawa amenaswa na kushindwa kuendelea na kazi yake ya uchawi” Aliieleza Mtanzania Media mmoja wa wananchi wa Jiji la Mwanza waliokuwa wakifuatilia tukio hilo kwa makini kabisa.

Taarifa za kudondoka kwa mwanamke huyo zimewaacha vinywa wazi watu waliokuwepo eneo la tukio, huku baadhi yao wakishindwa kutoa maelezo ya kina kuhusiana na tukio hilo ambapo baadhi yao wameamini kuwa mwanamke huyo ni mchawi kweli huku wengine wakishindwa kuamini na kudhania labda ni mtu tu ambae hana makazi maalumu na amekutwa maeneo hayo akiwa amejihifadhi. 

No comments:

Powered by Blogger.