NAMNA WATANGAZAJI NA WAFANYAKAZI WA RADIO METRO JIJINI MWANZA WANAVYOSAIDIA KUUKUZA UCHUMI WA TAIFA.
Wa kwanza kulia ni Dk.Tonny, Dj.Victor, Natty E, Sefcaren, Maria, Mamaa Lonah, Big Dad Oxs na Mpita Njia wako Frank M.Joackim. |
Kwa haraka haraka, Nikawazaaa na kuwazua nikagundua kuwa wafanyakazi hawa wanachangia pia pato la Taifa kuongezea ama hata kukua kwa namna moja ama nyingine. Hii ni kutokana na ukweli kwamba pesa yataka mzunguko na si kuitunza, sasa wao kwa kuwa ni sehemu ya kutengeneza pesa, wamempa mama mmoja mtalaamu wa mapishi ya kisasa kabisa jukumu la kuwaandalia chakula safi na chenye ubora kwa ajili ya mahitaji yao ya tumbo.
Pongezi kwa wote wanaofanya kama wafanyakazi wa Radio Metro, maana hii pia inaonyesha namna ya kuwaunga mkono akina mama zetu ambao wanajishughulisha na hivyo kuwaongezea kipato na hatimae maisha kusonga mbele.
No comments: