LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAZAMA KIKUNDI CHA LADIES FOR FUTURE KILIVYOIPENDEZESHA SHOW YA SATURDAY CLUB MIXING USIKU WA KUAMKIA LEO JIJINI MWANZA.

Hawa ni baadhi ya Wanachama wa Kikundi cha Akina dada Jijini Mwanza, kikundi ambacho kinafahamika kwa jina la LADIES FOR FUTURE. Kikundi hiki jana jumamosi June 14 kimetimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.

Baadhi ya majukumu ya Kikundi hiki ni pamoja na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile kujitolea katika shughuli za usafi Mahospitalini na maeneo mengine yenye uhitaji. Lakini pia mbali na kushiriki katika shughuli za kijamii, kikundi hiki kipo kwa ajili ya kuwezeshana (kukopeshana).

Pata time ya kutizama picha za wadada hawa (Ladies For Future) walipokuwa katika Show ya Saturday Club Mixing ya 99.4 Metro inayoruka hewani kila jumamosi kuanzia saa 22:00 hadi saa 01:00 usiku live kutoka katikati ya Jiji lenye Miamba, (Rock City-Mwanza) na Mwanaharakati wako George Binagi-GB Pazzo.
Baadhi ya Wanachama wa Kikundi cha Akina dada kinachofahamika kama Ladies For Future, wakiwa na furaha tele baada ya kutimiza mwaka mmoja jana tangu kuanzishwa kwa kikundi hicho, wenyewe wanasema ni wadada wanaojitambua.
Ngololo Ngololo, Ngololoooo...hapana chezea Ladies For Future.
Dada kapendeza sana na vazi lake la Kitenge, hakika vitenge vina raha yake.Tazama namna mavazi ya akida dada hawa yalivyowatoa fresh.
Jamani Metro Fm, unanifurahisha sana ndani ya nafsi yangu jamani
"Ngoja nione hii kama itakaa vizuri Intagramu"
Cheza cheza bila kukunja goti
Sugua gagaaa, sugua gagaaaaa
Kwa habari, Matukio na picha mbalimbali endelea kutembelea Mtanzania Media ili tufurahi pamoja nasi. Mtanzania Media; Kwa Pamoja, Tuijuze Jamii.

No comments:

Powered by Blogger.