LIVE STREAM ADS

Header Ads

MDAHALO MKUBWA WA WADAU WA ELIMU KUFANYIKA KESHO MKOANI MWANZA, IKIWA NI SEHEMU YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA.

 Kesho ni maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.Kimkoa katika Mkoa wa Mwanza Maadhimisho hayo yatafanyika katika Wilaya ya Magu, huku Wilaya nyingine nazo zikiadhimisha maadhimisho hayo katika Kiwilaya ambapo kutakuwa na shughuli mbalimbali kutoka kwa watoto.

Katika Wilaya ya Ilemela Maadhimisho hayo yatafanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Mh.Amina Masenza. Katika Wilaya ya Nyamagana Maadhimisho hayo yatafanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Buhongwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mh.Baraka Konisaga anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Kuanzia saa nane na nusu za mchana hadi saa kumi na mbili za jioni, katika Wilaya ya Nyamagana kutakuwa na Mdahalo Mkubwa ambao utafanyika katika Ukumbi wa Hotel ya JB Bell Monte ambapo wadau mbalimbali wa elimu wataweza mada tofauti tofauti kuhusiana na elimu katika Mkoa wa Mwanza. Kumbuka Kauli mbiu mwaka huu inasema kuwa "Kupata Elimu Bora na Isiyo na Vikwazo, Ni haki ya kila Mtoto"
Baadhi ya Watoto kutoka baraza la Watoto Mkoani Mwanza wakishow love na Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.