LIVE STREAM ADS

Header Ads

WASIWASI WA TANZANIA KUSHAMBULIWA NA AL-SHABAAB WATANDA. NI BAADA YA SERIKALI KURIDHIA KUTOA MAFUNZO YA KIJESHI KWA WANAJESHI WA SOMALIA.

Hali ya wasiwasi imeendelea kutanda hapa nchini miongoni mwa wananchi na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya Serikali ya Tanzania Kuridhia kutoa Mafunzo ya Kijeshi kwa Maaskari takribani 1,000 wa Somalia.

Tanzania imekubali kutoa mafunzo kwa askari wa Somalia kama sehemu ya jitihada zake kusaidia amani na usalama nchini Somalia, lakini baadhi ya maofisa wa Tanzania wameelezea wasiwasi kwamba Tanzania kujihusisha zaidi katika masuala ya Somalia kunaweza kukaribisha mashambulio ya kigaidi kutoka kwa al-Shabaab kama ilivyo kwa nchini Kenya.

Mapatano ya kutoa mafunzo kwa askari wa Somalia 1,000 kwa mara ya kwanza yalitolewa mwaka 2012, wakati Tanzania ilipokubali ombi la aliyekuwa rais wa Somalia Rais Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, ambalo tena limerudiwa na Rais Hassan Sheikh Mohamud mwaka huu.

"Tumeandaa makambi ya mafunzo na wakati huu ninapozungumza kila kitu kiko tayari. Tunasubiri kutoka kwao kuteua askari 1,000 kuja hapa kwa ajili ya mafunzo," alisema Salva Rweyemamu ambae ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa rais wa Tanzania na kuongeza "Tunasubiri kuwapa mafunzo kuwa askari wa kitaalamu ili kwamba wadumishe usalama wa nchi yao na kutoa fursa ya kujihusisha katika masuala ya maendeleo."

Akihutubia bunge may 21 mwaka huu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Tanzania Hussein Mwinyi alisema kuwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) limekuwa likiongoza katika kutoa mafunzo na operesheni za kulinda amani katika Afrika Mashariki na zaidi ya hapo kujenga ushirikiano imara wa kanda.

Mwaka uliopita, alisema TPDF ilitoa fursa za mafunzo kwa vikosi na maofisa wa jeshi kutoka Botswana, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia, Namibia, the Ushelisheli, Swaziland na Zimbabwe.
Pia alisema Tanzania awali iliwahi kutoa mafunzo kwa vikosi vya Somalia katika kutoa mwitiko wa ombi la Umoja wa Afrika, lakini hakusema ni vikosi vingapi vilipewa mafunzo au ni wakati gani ambapo alitaja operesheni nyingine ambazo Tanzania imekuwa ikizifanya kuwa ni pamoja na jukumu la kuongoza katika misheni ya kulinda amani ikiwa ni pamoja na Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo, Lebanon na Sudan Kusini.

Wakati serikali iliposema imejiandaa kutoa mafunzo kwa askari wa Somalia nchini Tanzania, wabunge na raia walitahadharisha dhidi ya kupanua misheni hiyo na kutuma vikosi nchini Somalia.

Job Ndugai, naibu spika wa Bunge la Tanzania, alisema ilikuwa ni hatari kubwa kwa usalama wa taifa kutuma vikosi nchini Somalia, ambavyo vingechochea uhasama wa al-Shabaab.
"Kwa hili nitakuwa mtu wa mwisho kuafiki," aliiambia Sabahi. " Angalia kinachoendelea nchini Kenya. Kwa hakika, serikali haipaswi hata kufikiria wazo la kupeleka vikosi nchini Somalia. Kama kitatokea chochote, tunapaswa kuwezesha mikutano kwa ajili ya pande zenye migogoro kusuluhisha tofauti zao." 

Mbunge Vincent Nyerere, wa chama cha upinzani Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alisema Tanzania inapaswa kufanya utafiti huru ili kuzingatia kama faida za kujihusisha katika mgogoro wa Somalia zinafaa. 

"Tunapaswa kujifunza kutoka kwa ndugu zetu wa Kenya," Alisema Kibamba na kuongeza "Awali Kenya haikuwa na uhasama na Somalia, lakini kwa kuingilia Somalia wanakabiliwa na mashambulio ya ugaidi (mara kwa mara) Tunapaswa kuepuka tatizo hilo."

Deus Kibamba, mkurugenzi mtendaji wa Idara ya Habari kwa Raia wa Tanzania, pia alisema serikali inapaswa kuepuka kujihusisha moja kwa moja katika mgogoro wa Somalia.
Alisema TPDF iliarifiwa kulinda mipaka ya Tanzania na raia wake, lakini mwelekeo wa sasa wa shughuli za amani unampa wasiwasi. 

"Ninadhani Tanzania hivi karibuni itazitumia rasilimali kupita kiasi kama tutajiingiza katika kila mgogoro unaotokea," alisema. "Tutaanzisha maadui na itakuwa shida kubwa kwa nchi yetu."

Lakini kwa upande mwingine Salva Rweyemamu ambae ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa rais wa Tanzania aliwahakikishia Watanzania kwamba serikali haitapeleka kabisa vikosi vyake nchini Somalia na kwamba hakujawa na maombi hayo kutoka Somalia wala Umoja wa Afrika mbali na ombi la kutoa mafunzo ya kijeshi kwa maaskari wa Somalia huku akitupilia mbali wasiwasi kwamba Tanzania itakuwa ikilengwa na al-Shabaab kwa kuisaidia serikali ya Somalia.

"Kumbukeni kuna serikali kamili nchini Somalia," alisema na kuongeza "Tanzania haitakuwa katika ukanda wa vita. Matakwa yetu, ambayo ni matakwa ya kila mmoja mwenye mawazo kama yetu, ni kuona amani inakuwepo nchini Somalia. Ni katika matakwa ya kila mmoja kurejesha amani nchini Somalia ikiwa ni pamoja na al-Shabaab."

Na Sabahi Online:

No comments:

Powered by Blogger.