BALOZI WA LIBYA NCHINI TANZANIA AJIUA KWA RISASI.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Assa Mwambene (Kulia).
Msemaji wa serikali hapa nchini Assa Mwambene amekiri kutokea kwa kifo cha Balozi Msaidizi wa Libya nchini bwana Ismail Nwairat kwa kujipiga risasi mwenyewe majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo katika chumba cha ofisi za ubalozi huo huku akiongeza kuwa mpaka sasa chanzo cha kifo cha balozi huyo hakijajulikana.

Baada ya balozi huyo kujipiga risasi walimuwahisha katika hospital ya Ami iliyopo Oysterbay na baada ya nusu saa madaktari walithibitisha kuwa amefarika dunia. Serikali imesikitishwa na kifo hicho na wanafanya utaratibu wote wa kuusafirisha mwili wa marehemu kuupeleka nchini kwao kwa ajili ya mazishi.
No comments: