LIVE STREAM ADS

Header Ads

HII NI FURSA NYINGINE INAYOTOLEWA NA BANK YA POSTA NCHINI TPB, HIVYO NI WAKATI WAKO KUICHANGAMKIA.

Henry Bwogi ambae ni Kaimu Mkurugenzi wa Mikopo kutoka Bank ya Posta nchini TPB Makao Makuu akiwa katika Studio za 99.4 Radio Metro ya Jijini Mwanza jioni ya leo, akizungumzia huduma Mpya ya Mikopo kwa Wastaafu ambayo inatolewa na Bank hiyo kwa hivi sasa ikiwa na RIBA NAFUU kabisa.
Shaban Tela Tela (Kushoto) ambae ni Meneja wa Bank ya Posta Tawi la Mwanza akiwa na Henry Bwogi (Kulia) ambae ni Kaimu Mkurugenzi wa Mikopo kutoka Bank ya Posta Makao Makuu Wakiwa katika Studio za Metro Fm Jijini Mwanza hii leo wakizungumzia huduma zinazotolewa na Bank ya Posta hapa nchini, hususani huduma Mpya ya Mikopo inayotolewa kwa Wastaafu hapa nchini na Bank hiyo.
"Bank ya Posta nchini inatoa huduma mbalimbali za Mikopo kwa riba nafuu ikiwa ni pamoja na Mikopo kwa ajili ya Biashara ambayo hutolewa kwa wafanyabiashara ya Kati na Kubwa, Mikopo Midogo Midogo kwa ajili ya Baba/ Mama ntilie, wenye biashara ndogo ndogo kama machinga nk. ambapo aina hii pia hutolewa kwa mtu mmoja mmoja ama vikundi vidogo vidogo. Pia aina nyingine ya Mkopo ni ile ya Mikopo binafsi kwa ajili ya wafanyakazi ama waajiriwa ambayo hutolewa kwa masharti nafuu kabisa na kubwa zaidi ni aina mpya kabisa kwa ajili ya Wastaafu ambapo hutolewa kwa wastaafu".
Bank ya Posta Nchini TPB inasifika kwa kutoa Mikopo mbalimbali kwa riba nafuu na kwa uharaka zaidi baada ya mwombaji kujaza fomu ya kuomba mkopo hivyo wananchi wanahamasishwa kuchangamkia fursa za kimikopo zinazotolewa na Bank hiyo kwa ajili ya kujiinua kiuchumi kupitia Mikopo inayotolewa na Bank hiyo. Zaidi wananchi wanashauriwa kutembelea matawi ya Bank hiyo kwa ajili ya maelezo zaidi juu ya huduma zinazotolewa na Bank ya Posta nchini ikiwa ni pamoja na Elimu ya Mkopaji bure kabisa, Mikopo ya haraka sanjari na huduma mbalimbali zinazotolewa kwa wateja wa Bank hiyo nchini kote.

No comments:

Powered by Blogger.