LIVE STREAM ADS

Header Ads

MICHUANO YA KOMBE LA MEYA KUANZA KUTIMUA MBIO ZAKE JIJINI MWANZA.

Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza na Diwani wa Kata ya Mkolani akizungumza hii leo juu ya Kuanza kwa Michuano ya Kombe la Meya Mwaka 2014. Michuano hiyo awali ilikuwa ikifahamika kama Pepsi Meya Cup.
Mashindano ya Kombe la Meya 2014 ambayo hapo awali yalikuwa yanafahamika kama Pepsi Meya’s Cup yanatajarajia kuanza hivi karibuni kwa kushirikisha jumla ya Timu 22 mwaka huu, kutoka Timu 19 zilizoshiriki mashindano hayo mwaka jana ikiwa ni ongezeko la Timu tatu zaidi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari hii leo, Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslauns Mabula ambae ni Mwanzilishi wa Mashindano hayo, ameeleza kuwa maandalizi yamekwisha kamilika na hivyo mashindano hayo yanatarajia kuanza mara baada ya Michuano ya Kombe la Dunia la FIFA kufikia tamati yake.
Mabula amebainisha kuwa Mashindano hayo yamepangwa kuanza kutimua mbio zake kuanzia tarehe 26 mwezi huu huku akiongeza kuwa Timu zote shiriki zinatarajiwa kupatiwa vifaa kwa ajili ya mashindano hayo tarehe 19 Mwezi huu katika Uwanja Mkongwe wa Nyamagana. Zaidi Mabula huyu hapa akielezea zaidi juu ya Michuano hiyo…

Katika hatua nyingine Mabula ameelezea kusikitishwa kwake na Ucheleweshwaji wa Ukarabati wa Uwanja Mkongwe wa Nyamagana kwa kuwekewa nyasi bandia, kama ilivyokuwa matarajio yake kwamba baadhi ya mechi za mashindano hayo mwaka huu zingechezewa katika Uwanja huo huku kukiwa na Nyasi bandia.
Kutokana na suala hilo la uwekaji wa nyasi bandia katika Uwanja huo wa Nyamagana kuonekana kama bado linasuasua, Mabula amepeleka kilio chake kwa TFF kuhakikisha kuwa suala hilo linafikia mwisho na hatimae uwanja huo kuwekewa nyasi bandia.
Itakumbukwa kuwa Michuano ya Kombe la Meya inajumuisha Timu kutoka katika Kata zote 12 za Jiji la Mwanza na kwa Mujibu Mstahiki Meya wa Jiji Mwanza ni Kwamba Michuano hii ya Kombe la Meya inazidi kuboreshwa na katika Mikoa Mingine ili hatimae iweze kutoa fursa kwa washindi wa mikoa hiyo kukutana na kuchuana kwa ajili ya kumpata bingwa wa Kombe la Meya ngazi ya Taifa.

No comments:

Powered by Blogger.