LIVE STREAM ADS

Header Ads

VITAMBULISHO VYA ZAMANI VYA KUPIGIA KURA KUTOTUMIKA TENA. TUME TAIFA YA UCHAGUZI YAWATAKA WANANCHI KUJIANDAA NA MABADILIKO HAYO.

Mkuu wa Idara ya Uchaguzi NEC Mh. Bi. Clotilda Komba (Kushoto) na Kamishina wa Uchaguzi NEC Mh. Bi. Mchanga Mjaka (Kulia) wakiwa katika Mkutano na Waandishi wa Habari Mkoani Mwanza.Mkutano huo umefanyika hii leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imetoa rai kwa wananchi kujiandaa na zoezi la Uboreshaji wa daftari la Kudumu la Wapiga Kura, ambalo litarajia kuanza hivi karibuni kwa kutumia mfumo mpya wa Teknolojia wa Biometric Voter Registration BVR.

Hayo yameelezwa hii leo na Mchanga Mjaka ambae ni Kamishina wa Tume hiyo katika Mkutano na Waandishi wa Habari Mkoani Mwanza, kuhusu Uboreshaji wa daftari la kudumu la Wapiga Kura unaotarajia kuanza Mapema Mwezi Septemba Mwaka huu.
Mchanga amesema kuwa Mfumo wa Biometric Voter Ragistration BVR ni mfumo wa kuchukua taarifa za mwanadamu za kibailojia na kuzihifadhi katika kanzi data kwa ajili ya utambuzi ambapo mfumo huo hutumika pia katika kumtambua mtu na kumtofautisha na mtu mwingine.

Aidha amebainisha kuwa Tume imefanya maamuzi ya kutumia mfumo huo mpya wa BVR katika kuboresha daftri la Wapiga kura, kutokana na changamoto zilizojitokeza katika mfumo wa zamani wa Optical Mark Recognition OMR ambao ulisababisha kwa kiasi kikubwa daftari la kudumu la Wapiga kura kuwa na kasoro.
                        Maryam Ukwaju ambae ni Afisa Uchaguzi kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Ameongeza kuwa Tume ina mategemeo makubwa kwamba Matumizi ya Mfumo huo mpya wa BVR yatapunguza ama kuondoa kabisa matatizo yaliyojitokeza katika daftari lililopo la wapiga kura ambapo amewahimiza wananchi kujiandaa na maboresho hayo ambayo yatatoa fursa ya kuwepo kwa vitambulisho vipya vya kupigia kura na hivyo kuondoa matumizi ya vitambulisho vya sasa.
                                                 
Katika hatua nyingine Mjaka amebainisha kuwa uhakiki wa vituo vya kuandikishia wapiga kura umeishafanyika, na kwamba hivi sasa uandikishaji unatarajia kufanyika katika ngazi ya vitongoji, vijiji na mitaa tofauti na awali ambapo vituo vilikuwa katika ngazi ya Kata pekee.
                                         Rose Malo ambae ni Afisa Elimu ya Mpiga Kura.

Kutokana na mabadiliko hayo, vituo vya kujiandikishia vimeongezeka kutoka 24, 919 hadi kufikia 40,015 jambo ambalo litapunguza malalamiko ya umbali wa vituo vya kujiandikishia na hivyo kuongeza mwamko kwa wananchi kujitokeza kujiandikisha na kupiga kura.
                                                
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Uchaguzi Kutoka NEC Clotilda Komba ameeleza kuwa zoezi hilo la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linahusisha Uandikishaji wa Wapiga Kura wapya ambao ni raia wa Tanzania waliotimiza umri wa miaka 18 na kuendelea na wale ambao kutokana na sababu mbalimbali hawakuweza kujiandikisha hapo awali.
Aidha ameongeza kuwa zoezi hilo litahusisha uondoaji wa majina ya wale ambao wamepoteza sifa ya kupiga kura kwa mjibu wa sheria na wale ambao wamefariki sanjari na wale ambao wamehama kutoka Kijiji, Mtaa, Kata ama jimbo la awali na kwenda jimbo jingine.
                                                 
Inatarajiwa kwamba vitambulisho vipya vitakavyopatikana baada ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, ndivyo vitakavyotumika katika zoezi la upigaji kura ya maoni ya kupata Katiba Mpya na katika uchaguzi mkuu ujao wa Mwaka 2015, ambapo zoezi la uboreshaji wa daftari hilo linatarajiwa kukamilika ndani ya siku 14 mwezi September Mwaka huu.
Waandishi wa Habari.(Picha zote chini ni Wana habari walioshiriki katika Mkutano huo).

No comments:

Powered by Blogger.