LIVE STREAM ADS

Header Ads

USIYOYAJUA KUHUSU BUNGE LA BAJETI LILILOHITIMISHWA HIVI KARIBUNI MJINI DODOMA.

Dk.Kenny Salvatory ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya The Voice Of Youth Club yenye Makao Makuu yake Mkoani Mwanza akiwa katika Studio za 99.4 Metro Fm Jijini Mwanza. Taasisi hii inahusika zaidi na Utoaji wa Elimu ya Uelewa na Uwajibikaji kwa Vijana na Jamii kwa Ujumla. Akiwa katika Kipindi cha Pambazuko la Metro Fm asubuhi ya Leo, Dk.Kenny amejaribu kuzungumzia Bunge la Bajeti lililomalizika hivi karibuni ukizingatia kwamba yeye alipata fursa ya kuhudhuria Mijadala na vikao vya Bunge hilo Mjini Dodoma.





Dk.Kenny amegusia baadhi ya Maeneo ambayo amesema kuwa siku zote hulifanya bunge la bajeti kuwa tofauti kidogo na Mabunge Mengine. Moja ya Maeneo aliyosasema ni Pamoja na Eneo la Serikali ambapo hapa viongozi wa Serikali kama vile mawaziri huwa na kazi ya ziada katika Kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa bajeti iliyopita sanjari na kuinadi bajeti ijayo. Anasema katika eneo hili Mawaziri huumiza vichwa sana katika kuwaeleza wananchi namna walivyofanikiwa kutimiza ahadi za bajeti iliyopita katika wizara husika sanjari na kuja na ushawishi wa kuwaeleza kwa maeneo ambayo ahadi haikutimizwa na namna ya kutimiza ahadi zao.

Eneo jingine alilosema Dk.Kenny ni Eneo la Wabunge, ambapo eneo hili huwa wabunge wengi wamejipanga katika kuihoji Serikali juu ya ahadi zake katika bajeti iliyopita na kutaka kujua namna ahadi hizo zilivyotekelezwa ama laa na kwa nini hazikutekelezwa. Anasema katika Eneo hili wananchi nao huwa wako makini sana kufuatilia kwa makini kujua ni nini wabunge wao watachangia ama kuihoji Serikali juu ya maendeleo ya majimbo yao.

Alphonce Tonny Kapella aka Dk.Tonny akiwa ndani ya Pambazuko la Metro Fm.

Pia anasema Bunge la Bajeti ni Bunge ambalo kila mmoja katika jamii hutaka kujua ni nini kitazungumzwa ama kujadiliwa.Wengi hutaka kujua kama kodi itapanda ama kupungua, Mishahara itaongezeka ama laa, Je kodi itapanda au itapungua. Anasema ni Bunge ambalo kila mwananchi huwa yuko tumbo joto kutaka kujua kila jambo linalowasilishwa na kujadiliwa.

Kwa upande mwingine pia Dk.Kenny anasema kuwa amegundua kwamba Bunge la Bajeti ni Bunge ambalo hata wawekezaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi hulifuatilia kwa lengo la kutaka kujua ni maeneo gani ya kiuwekezaji ambayo Serikali imeyapa kipaumbele ili kuweza kutumia fursa hiyo kwa ajili ya uwekezaji. Kwa ujumla anasema Bunge la Bajeti si bunge ambalo hufuatiliwa nchini tu bali duniani kote kulingana na umhimu wake.

Kenny Salvatory (Kushoto), Alex Ngusa (katikati) na Mc.Katumba (Kulia) katika Studio za Metro FM.

Kuhusiana na Bajeti Tegemezi ambayo imekuwa ikilalamikiwa hapa nchini, Dk.Kenny anasema kuwa hilo haliwezi kuepukika hata siku moja kwa hivi sasa na hata katika siku za hivi karibuni (Zijazo) kwa kuwa asilimia kubwa ya watanzania hawalipi kodi ikizingatiwa kwamba uchumi wa mataifa hutegemea kodi kwa asilimia kubwa.

"Kwa Mfano chukulia kwamba Watanzania wanaopaswa kulipa kodi ni Milioni 25, Matokeo yake utakuta Watanzania Milioni Tano pekee ndio wanaolipa kodi, sasa kwa hali hii lazima bajeti yetu itaendelea kuwa tegemezi na Taifa litajikuta likiendelea kuongeza deni la Taifa kwa kuwa hakutakuwa na namna ya kujinusuru zaidi ya kutegemea Wahisani na kuendelea kukopa. Na hii ndiyo ambayo imekuwa ikisababisha wafanyakazi Kila Siku kulalamikia Kodi kubwa wanayokatwa kwa kuwa asilimia kubwa wao ndio wanaolipa kodi”.

No comments:

Powered by Blogger.