DK.MAGUFULI KUZINDUA KIVUKO KIPYA JIJINI MWANZA. FOLENI SASA BYE BYE.
Wananchi na Wakazi wa Jiji la Mwanza
wanatarajia Kuepukana na Usumbufu
wa Foleni za Barabarani wanaokumbana nao hususani Majira ya
Asubuhi na Jioni, Baada
ya Waziri wa Ujenzi Dk.John Pombe Magufuli kutimiza ahadi ya Serikali kuleta Kivuko Jijini Mwanza kwa ajili
ya kupambana na Foleni hizo.
Kivuko hicho ambacho kinatarajiwa
Kuzinduliwa Kesho na Dk.Magufuli kitakuwa kikifanya Safari zake katika mwambao wa Ziwa Victoria kuanzia eneo la Luchelele Kupitia Sweya,
Butimba, Mkuyuni, Igogo na hatimae Kirumba na hivyo kusaidia wananchi wa Jiji
la Mwanza Kuepukana na Changamoto za Foleni za barabarani.
Taarifa kutoka Kitengo cha Mawasiliano,
Wizara ya Ujenzi kwenda kwa Vyombo vya Habari zimeeleza kuwa Kivuko Hicho
kitakuwa na uwezo wa Kusafiri kwa mwendo kasi, kwa lengo la
kutoa huduma ya Usafiri kwa uharaka zaidi huku kikiwa na Uwezo wa Kubeba Tani 65 ambazo ni sawa na abiria 80 na Magari madogo matano
kwa wakati Mmoja.
Japo bado gharama za Usafiri katika
Kivuko hicho hazijawekwa wazi hadi pale kitakapozinduliwa Siku ya Kesho na
Dk.Magufuli, Kivuko hicho kinatarajiwa kuwa Mkombozi kwa wananchi wa Jiji la
Mwanza ambalo linakuwa kwa kasi kubwa na kusababisha Foleni kuanza kuwa kero kwa
wasafiri wake kutokana na kutumia masaa mengi wakiwa
barabarani wakati wa kwenda
ama kutoka Makazini.
Kivuko hicho kitafahamika kwa Jina la
MV.TEMESA na kitakuwa chini ya Usimamizi wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania
(TEMESA), ambapo kesho TEMESA
inatarajia kutangaza gharama za Usafiri katika
Kifuko hicho huku Siku ya Kwanza baada ya Kuzinduliwa kwake Wananchi wakitarajia kutumia Kivuko hicho bure.
No comments: