LIVE STREAM ADS

Header Ads

JAJI MUTUNGI ASEMA SIKU ZA MWIZI NI AROBAINI. ASEMA IPO SIKU CHADEMA WATAUMBUKA HADHARANI.



Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, amesema hana haja ya kuhangaika na tuhuma zilizotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwa ofisi yake inatumiwa ili kukisambaratisha chama hicho.


Amewataka Watanzania watulie na ukweli utabainika tu, ikizingatiwa siku za mwizi ni arobaini. Jaji Mutungi alisema hayo jana, alipozungumza na MTANZANIA kuhusu tuhuma zilizoelekezwa katika ofisi yake na Chadema.

Jaji Mutungi ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku mbili baada ya Chadema kumtaka ajitokeze hadharani kubainisha ukweli iwapo yeye ndiye aliyemtuma msaidizi wake, Sisty Nyahoza kusema kuwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, hana sifa ya kugombea uongozi ndani ya chama hicho kutokana na kuzuiwa na Katiba ya Chadema.

Nyahoza alikaririwa na vyombo vya habari hivi karibuni akisema Mbowe hana sifa za kugombea uongozi wa chama hicho, kwa vile katiba ya chama hicho inambana. Alisema kipengele cha ukomo wa mgombea katika katiba Chadema ya mwaka 2006 kiliondolewa kinyemela bila idhini ya mkutano mkuu.

Nyahoza alisema katiba ya Chadema ya mwaka 2004 ilikuwa na kipengele cha ukomo wa madaraka kilichoeleza kuwa kiongozi aliyeongoza vipindi viwili vya miaka mitano mitano hawezi kuwania tena nafasi hiyo. Mvutano huo ulikifanya chama hicho kumlaumu Msajili, Jaji Mutungi, kikidai ofisi yake inatumiwa na wasaliti wa chama hicho.
 
Julai mosi, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, alisema Jaji Mutungi hana mamlaka ya kubaini sifa za viongozi wa chama hicho, bali wenye mamlaka hayo ni wanachama wa chama hicho pekee. Mnyika alisema mwaka 2006, katiba ya Chadema haikurekebishwa, bali iliundwa upya na kuridhiwa na mkutano mkuu wa chama na kwamba Agosti 13, 2006 ilizinduliwa na nyaraka zote alikabidhiwa Msajili wa Vyama wa wakati huo, John Tendwa.
 
Alisema katika mchakato huo yalikuwapo mabishano na makubaliano katika baadhi ya masuala, lakini suala la ukomo wa uongozi liliafikiwa na wanachama wote bila tatizo na kupitishwa kuingizwa katika katiba na Ofisi ya Msajili ilipelekewa fomu ya marekebisho na katiba mpya kama sheria inavyotaka.

No comments:

Powered by Blogger.