LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMA USHAURI HUU HAUTAZINGATIWA, KUNA HATARI YA MAASKARI WA ULINZI KUSHIRIKIANA NA WAHALIFU HAPA NCHINI.

Soma na Tazama picha za Maaskari wa Kampuni ya Ulinzi ya KK.Security ambao wamehitimu Mafunzo yao ya Ulinzi hii leo katika Uwanja Mkongwe wa Nyamagana Mkoani Mwanza.

Makampuni mbalimbali ya Ulinzi na Usalama hapa nchini yameshauriwa Kuzingatia Maslahi bora kwa Maaskari wake, ili kuwawezesha Maaskari hao kuondokana na Vishawishi wanavyoweza kuvipata katika maeneo yao ya kazi na kujikuta wakishirikiana na waharifu kutokana na Ugumu wa Maisha.


Ushauri huo umetolewa hii leo Jijini Mwanza na Meneja wa Kampuni ya Ulinzi ya KK.Security Kanda ya Ziwa Levina Vedasto Beal, wakati akizungumza na Radio Metro kufuatia Maaskari wa Kampuni hiyo kuhitimu mafunzo yao hii leo katika Uwanja wa Nyamagana Mkoani Mwanza.

Amesema Maslahi duni kwa maaskari kutoka kwa baadhi ya Makampuni ya Ulinzi hapa nchini ni changamoto kubwa, hali ambayo ni hatari kwa kuwa inaweza kuongeza kiwango cha uharifu katika maeneo mbalimbali ambayo yanalindwa na maaskari hayo.


Aidha amebainisha kuwa kwa Upande wa Kampuni ya KK.Security suala la maslahi wamelibaini na wanalizingatia kwa kuwalipa maaskari na watumishi wa Kampuni hiyo kwa ujumla kwa mjibu wa Viwango vya Mishahara vilivyowekwa na Serikali na hata wakati mwingine kwenda zaidi ya Viwango hivyo kwa ajili ya Kuimarisha utendaji kazi wa wafanyakazi wake.

Kwa Upande wa baadhi ya Wahitimu wa Mafunzo hayo wameelezea furaha yao baada ya kuhitimu mafunzo ya Ulinzi yanayotolewa na Kampuni hiyo, kwa kusema kuwa  mafunzo hayo yatawapatia fursa ya kujipatia ajira na hivyo kuondokana na tatizo la ajira ambalo lilikuwa likiwakabili hapo awali kabla ya kupata mafunzo hayo.


Aidha wamewashauri vijana wengine kuchangamkia nafasi za Ulinzi zinazotolewa na Kampuni ya  KK.Security Kote nchini ili kuweza kuondokana na Changamoto ya Upatikanaji wa ajira, kwa kuwa Kampuni hiyo imekuwa ikichangia kwa sehemu kubwa katika kutoa ajira kwa Vijana huku wakiahidi kuyatumia vyema mafunzo hayo kwa kuzingatia maadili ili kuimalisha ulinzi na usalama katika jamii.

Jumla ya Wahitimu 35 kati ya 40 wote wakiwa ni wanaume ambao walijiunga na mafunzo hayo ya Ulinzi wamehitimu hii leo, huku wengine watano wakishindwa kuhitimu kutokana na Sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushindwa kumdumu mafunzo yanayotolewa na Kampuni hiyo ambapo zaidi ya Wahitimu 60 wamekuwa wakihitimu mafunzo hayo kila mwezi kutokana na awamu mbili za mafunzo ambazo hutolewa kila mwezi kwa kujumuisha zaidi ya wahitimu 30 kila awamu.















Meneja wa Kampuni ya Ulinzi KK.Secury Kanda ya Ziwa Levina Vedasto Beal.

No comments:

Powered by Blogger.