LIVE STREAM ADS

Header Ads

SASA TUNAINGIA TARIME. TAZAMA WANAFUNZI WA REBU SEKONDARI WALIVYOTISHA KATIKA MAHAFALI YAO.

Haya ni Mahafali ya Sita ya Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Rebu iliyoko Kata ya Turwa Wilaya Tarime Mkoani Mara. Mahafali haya yalifanyika Mwaka jana October 18 katika Viwanja vya Shule hiyo. Ni Mahafali ambayo yalivuta hisia za wanafunzi wengi wa Shule hiyo ikizingatiwa kwamba wanafunzi waliohitimu Kidato cha nne Shuleni hapo Mwaka 2012 hawakuweza kufanya Mahafali yao kutokana na Sababu mbalimbali jambo ambalo lilifanya Mahafali haya kunoga zaidi kwa kuwa Wanafunzi wa Shule hiyo ni kama waliumizwa na kitendo cha Mahafali ya mwaka 2012 kutokufanyika.
Mtanzania Media inawatakia utazamaji mwema wa picha hizi hususani wote waliohitimu Kidato cha nne mwaka jana Shuleni hapo sanjari na wanafunzi wote waliohitimu kidato cha nne shule hapo. Kumbuka hata George Binagi ambae ni Mtangazaji na Mwandishi wa Habari kutoka 99.4 Radio Metro ya Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Blog hii ya Mtanzania Media ni ZAO la Rebu Sekondari. Mahafali ya Kwanza Shuleni hapo yalifanyika Mwaka 2008 na hivyo hadi kufikia mwaka jana 2013 zimenyafika Mahafali Tano huku moja ya mwaka 2012 ikishindwa kufanyika kutokana na sababu mbalimbali.
Ahsante kwa kutembelea Mtanzania Media, Ungana nasi mara kwa mara kwa ajili ya kupata Habari na Matukio mbalimbali. Share ili na wenzako waweze kutizama picha hizi maana ni kumbukumbu nzuri sana.

No comments:

Powered by Blogger.