LIVE STREAM ADS

Header Ads

SWEET CAKE KAAMUA KUACHIA WIMBO WAKE, BAADA YA KUONA DIAMOND ANAMCHELEWESHA.

Sweet Cake
Msanii Sweet Cake kutoka Jijini Mwanza ameamua kuachia Ngoma yake mpya ambayo inakwenda kwa jina la ULISEMA UTAREJEA, ambapo humo ndani ni kama amemjibu Diamond Platnum katika Wimbo ambao ulimuweka kwenye ramani ya Muziki.

June 22 Mwaka huu akipiga Story na George Binagi-GB Pazzo ndani ya Studio za Metro FM, Sweet Cake alisema kuwa amepata baraka zote kutoka kwa Diamond juu ya kufanya ngoma hiyo ambapo Diamond alimuahidi kuweka mistari yake katika huo wimbo.

Lakini kutokana na sababu ambazo Sweet Cake alizieleza kuwa ni Mishe nyingi za Platnum, Ngoma hiyo imeshindwa kukamilika kwa wakati hali ambayo imemlazimu jamaa kumpa shavu katika huo wimbo Abuu Mkalii katika Verse ambayo Platnum angesimama, huku akiahidi kuwa kama mambo yataenda sawa basi Wimbo huo wa Ulisema Utarejea atakuja kuurudia tena pale Platnum atakapoingiza voko zake.

Pata time ya kuusikiliza Wimbo huu, ambao yeye anasema si kwamba karudia wimbo wa Platnum bali kamjibu Platnum>>>.SI ULISEMA! Mawasiliano...0769 60 83 62

Na:George Binagi @99.4 METRO FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.