LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAFANYABIASHARA MKOANI MWANZA WAGOMEA MKUTANO WA JUMUIYA WA WAFANYABIASHA TANZANIA.

Mchungaji Silver Kionda ambae ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoani Dodoma na Mikoa ya Kanda ya Kati.

Mkutano wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Tawi la Mwanza, jana Umeshindwa kufanyika baada ya Wafanyabiashara wanaounda Jumuiya hiyo Kushindwa kuhudhuria Mkutano huo ambao ulikuwa umeitishwa na Uongozi wa Jumuiya hiyo Tawi la Mwanza.


Mkutano huo ambao ulikuwa umepangwa kufanyika katika Ukumbi wa Aspen Hotel Jijini Mwanza, Ulikuwa umelenga Kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara, sanjari na Viongozi wa Jumuiya hiyo kuwasilisha taarifa mbalimbali juu ya malalamiko ya Wafanyabiashara ambayo wamekuwa wakiyaelekeza kwa Serikali na namna yalivyoshughulikiwa na Jumuiya.


Akizungumza kabla ya kuahirishwa kwa Mkutano huo, Mchungaji Silver Kiondo ambae ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoani Dodoma, ambae alikuwa Mgeni Rasmi  ameelezea kusikitishwa na kitendo cha Wafanyabiashara Mkoani Mwanza kutohudhuria Mkutano huo kwa kubainisha kwamba hatua hiyo inahatarisha uhai wa Wafanyabiashara Mkoani Mwanza.


Katika Maelezo yake, Mchungaji Kionda amebainisha kwamba hatua hiyo inaonyesha kuwa malalamiko ambayo Jumuiya imekuwa ikiyazungumza Serikalini hayatoki kwa Wafanyabiashara bali yanatoka kwa viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania.

Miongoni mwa Mambo ambayo yalikuwa yanatarajiwa kutolewa Ufafanuzi katika Mkutano huo ni pamoja na Matumizi ya Mashine za Kutolea Stakabadhi (EDF’S) na namna ambavyo Jumuiya imekuwa ikishughulikia Malalamiko ya Wafanyabiashara kuhusiana na Matumizi ya Mashine hizo.


Akiahirisha Mkutano huo, Mchungaji Kionda ameishauri Mamlaka ya Mapato nchini TRA, kuhakikisha inawashughulikia Wafanyabiashara wote ambao bado hawajanunua Mashine za EFD’S, hii ikiwa ni baada ya Wafanyabiashara Mkoani Mwanza kutohudhuria Mkutano ambao ungejadili na kutoa taarifa kuhusiana na Matumizi ya Mashine hizo.

            Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoani Mwanza Christopher Wambura.


Baada ya Mkutano huo kuahirishwa, Ikamlazimu Mchungaji Kiondo kuzungmza na Waandishi wa Habari na kuelezea kile ambacho alikuwa amepanga kukieleza kwa Wafanyabiashara wanaounda Jumuia ya Wafanyabiashara Mkoani Mwanza.


Katika Maelezo yake akabainisha kuwa alitaka kuzungumzia Mfumo wa Utozaji wa kodi hapa nchini kwa kutumia mashine za EFD’S, ambapo alibainisha kuwa mfumo huo ulianzishwa kwa nia njema ya kuisaidia Serikali katika kukusanya kodi na kuzuia ukwepaji kodi kwa ajili ya kuongeza makusanyo ya kodi nchini.


Tofauti na Mantiki hiyo, Mchungaji Kiondo akauita Mfumo huo kuwa ni mfumo mbovu na ambao unahitaji mabadiliko kwa kuwa matumizi ya mashine hizo kwa hivi sasa yamelenga kumfirisi mfanyabiashara, ambapo TRA imekuwa ikiidanganya Serikali na Umma juu ya Matumizi ya Mashine hizo ili Jumuiya ya Wafanyabiashara ionekane inakataa kutumia mashine za EFD’S.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Patrick Masagati (Kulia) Akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Dodoma (Kushoto) baada ya Mkutano Kuahirishwa jana.
 
Hii ndiyo ilikuwa Taswira ya Mkutano jambo ambalo lilionekana kumchefua Mgeni Rasmi Mchngaji Silver Kionda ambae ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoani Dodoma na Mikoa ya Kanda Kati ambapo alisema kamwe hawezi kurudi tena Mkoani Mwanza tena Kuzungumza na Wafanyabiashara.
MSIKILIZE HAPA MCHUNGAJI KIONDO WAKATI AKIAHIRISHA MKUTANO.


MSIKILIZE HAPA MCHUNGAJI KIONDO WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI.

Na: George Binagi @99.4 Radio Metro & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.