LIVE STREAM ADS

Header Ads

TOFAUTI KATI YA MSOMI NA MWENYE ELIMU.

                  Kennysalfes Salvatory, Mwenyekiti wa The Voice OF Youth Club-Mwanza.  
Mwenye elimu ni yeyote asiyemjinga katika eneo flani[yaani uelewa/ufahamu juu ya matumizi n.k ya kitu ama jambo flani] elimu si lazima itolewe darasani ndiyo maana kuna kitu kinaitwa elimu dunia,hivyo mtu akikuita mjinga kabla hujakasirika furahia ila umuulize mimi mjinga eneo gani? 
Kwa kuwa nimekwambia mtu kuwa mjinga ni hali ya kutokuwa na uelewa/ufahamu wa jambo ama kitu flani.2 MSOMI NI MTU MWENYE UJUZI/TAALUMA FLAN I juu ya jambo flani,kwa maana nyingine huwezi kuitwa msomi kama hujabobea katika tasnia husika,inaweza ikawa katika mambo ya siasa,uhandisi,kilimo,sayansi,dini n.k,ndiyo maana makazini watu huajiliwa kwa utalamu wao[yaani taaluma zao] 
Ngoja niseme hivi ili uelewe zaidi,wasomi wako kwa ajiri ya kutatua matatizo kwa kuwa wamebobea katika maeneo husika mfano madaktari..ndiyo maana wakati flani unaweza kusikia tuna uhaba wa wataalamu,wenye elimu ni wengi kuliko wataalamu,NAOMBA NIMALIZE HIVI,MTU ANAWEZA KUWA NA UELEWA WA SHERIA LAKINI ASIITWE MWANASHERIA...
UMENIELEWA MPENDWA? Haya nikupe na huu mfano wa mwisho,kama ukiwa hujui kutumia kompyuta kwa lugha nyepesi niseme wewe ni mjinga katika eneo hilo la matumizi ya kompyuta,lakini ukipata maelekezo ya matumizi yake hautaitwa tena mjinga ila utaitwa una una ufahamu yaani elimu ya kompyuta lakini kamwe hauwezi kuitwa MTALAAMU WA KOMPYUTA.
Namaliza kwa mnyumbuisho wa maneno yafuatayo. 1.ELIMU-elimika-elimisha-elimishwa. 2.SOMO-soma- someka- someshwa-somea- USOMI- MSOMI. 3.TAALAMU-taluma-mtalam.AKSANTENI SANA KWA KUNIELEWA,NA PIA NAWASHUKURUNI KWA KUWA MNANIANDAA KUWA KIONGOZI BORA WAKATI UKIWADIA.
Na: Kennysalfes Salvatory.

No comments:

Powered by Blogger.