LIVE STREAM ADS

Header Ads

HII NI FURSA KWA WOTE. NI JUMAMOSI HII NDANI YA CHUO KIKUU SAUT MKOANI MWANZA.

Selma Boeke (Kushoto) kutoka nchini Holland akiwa na Carolline Persson (Kulia) kutoka nchini Swiden wakiwa katika Studio za 99.4 Metro Fm.Wao wanatoka Tasisi ya AIESEC na wanafanya kazi ya Kujitolea na Kampuni ya PSP Mwezeshaji Consultancy.
Baada ya Wajasiriamali Mkoani mwanza Kushindanishwa katika Makundi Manne juu ya Uandaaji wa Wazo/Mpango ya Biashara chini ya Usimamizi wa PSP Mwezeshaji Consultancy kwa Kushirikiana na Taasisi ya AIESEC, Mshindi anatarajiwa kupatika Jumamosi hii ya July 26 kuanzia saa Saba mchana hadi saa Kumi Alasiri katika Ukumbi wa Mwanjonde Lecture uliopo katika Chuo Kikuu cha SAUT, ambapo pia kutakuwa na Zawadi kwa Washindi ambazo zitakabidhiwa na Mgeni Rasmi. Mbali na hayo pia Siku hiyo Wajasiriamali wadogo, wa Kati na Wakubwa watapata fursa ya Kupata elimu ya Biashara Bure kabisa....kwa Ufupi ni Kwamba HAKUNA KIINGILIO.
Sefroza Joseph, Mtangazaji wa Metro FM (Kushoto) akifuatiwa na Selma Boeke (Katikati) kutoka nchini Holland akiwa na Carolline Persson (Kulia) kutoka nchini Swiden wakiwa katika Studio za 99.4 Metro Fm.
Protase Salus Semuhomyi Mkurugenzi Mtendaji wa PSP Mwezeshaji Consultancy (Kushoto),
Selma Boeke (Katikati) kutoka nchini Holland akiwa na Carolline Persson (Kulia) kutoka nchini Swiden.Mwenye Kofia ni CEO wa Mtanzania Media na Mtangazaji wa Metro FM George Binagi-GB Pazzo.

Protase Salus Semuhomyi Mkurugenzi Mtendaji wa PSP Mwezeshaji Consultancy akiwa Metro FM akizungumzia Event inayoratajiwa Kufanyika Jumamosi hii ya July 26 katika Viunga vya Chuo Kikuu cha SAUT. Itakuwa ni Fursa kwako wewe Mjasiriamali maana unaambiwa "Kila Kikubwa, Kilianza Kama Kidogo" hata WEWE unaweza pia. Kwa Mawasiliano zaidi piga simu namba 0784 69 07 12 AU 0753 77 85 71.
Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.