LIVE STREAM ADS

Header Ads

JIJI LA MWANZA LAJIPANGA KUKABILIANA NA ONGEZEKO LA UCHAFU.

                   Afisa  Afya Jiji la Mwanza Danford Kamanya.
Halmashauri ya Jiji la Mwanza imeongeza  magari  tisa ili kukabiliana na  changamoto ya kuchelewa kuondolewa kwa Taka  katika kutekeleza jukumu la kuwa na sifa ya usafi wa mazingira kama ilivyo ada.
Hii ni kutokana na kuwepo kwa ongezeko kubwa la uzalishaji wa  taka ngumu  katika maeneo mbalimbali jijini hapa na  swala ambalo litasababisha maeneo yaliyotengwa kwaajili ya kuwekwa taka kujaa haraka.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Afisa  Afya Jiji Danford Kamanya alieleza kwamba kutokana na kuwepo kwa uzalishaji huo, Halmashauri ya jiji kwa kushirikiana na wazabuni mbalimbali, imeongeza idadi ya magari ya utoaji taka katika maeneo yaliyotengwa ili kuhakikisha Jiji linaendelea kuwa safi kwa  miaka ijayo .
Alieleza kuwa magari hayo yataongeza utendaji kazi wa kusafisha mazingira ikiwa ni pamoja na kuepuka ukaaji wa takataka kwa muda mrefu kwenye maeneo ya ukusanyaji  yaliyotengwa na Halimashauri ya Jiji.
“Jukumu la ukusanyaji  wa taka Jijini hapa umeboreshwa kwa ushirikiano wa Halmashauri  na wazabuni ,hivyo kuondokana  na adha iliyopo” Alisema Kamanya.
Kamanya aliwaomba wafanyabiashara na wakazi  wa jiji kuacha tabia ya kutupa taka ovyo bali wazipeleke  taka katika maeneo yaliyotengwa ili kuepukana  na uchafuzi wa  mazingira katikati ya jiji.
Na: Prisca Japhes

No comments:

Powered by Blogger.