LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MAADILI YANAYOFAA.

UMOJA wa wanawake Tanzania (UWT),umewataka wazazi na walezi Mkoani  Mwanza kuwalea watoto katika maadili mema kama ilivyo kuwa zamani.
Akizungumza  na  umoja huo katika kata ya Igoma Jijini Mwanza, Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Asha Abdallah alieleza kuwa, wazazi na walezi walio wengi ,wamesahau kuwalea watoto wao katika maadili yanayo faa, hivyo kuwafanya wajiingize katika vitendo viovu ikiwa ni pamoja na uvutaji bangi.

“Watoto hawafuati maadili kama ilivyokuwa zamani na sisi wazazi tupo tunawaangalia tu, wanawake wenzangu ifike mahali tubadilike  na tuwalee watoto wetu katika maadili yanayo kubalika katika jamii” Alisema Asha.

Alieleza kwamba maadili yanayotakiwa, ni pamoja na kuangalia mavazi  ya watoto  wanayovaa, watoto wa kike kurudi nyumbani mapema kama ilivyokuwa zamani ambapo watoto wakike ilikuwa mwisho saa 12 jioni kurudi nyumbani.

“wazazi wa siku hizi tumekuwa wakimya mno, mtoto wa kike anafika saa mbili za usiku hata kumuuliza alikuwa wapi hamna,na  akija na kitu ambacho haujamnunulia wewe haumuulizi hata kama unajua hana kipato chochote cha kumfanya anunue kitu hicho jamani tun awapeleka wapi watoto. Alieleza na kuongeza kuwa,

Yote hayo ndio yanayo sababisha ongezeko la mimba za utotoni ambazo zimekuwa ni tatizo kwa watoto wa kike wa kizazi cha sasa.  
Aliongeza kuwa , idadi kubwa ya wazazi  kwa sasa wanajali mambo yao binafsi ikiwa ni pamoja na kutafuta pesa na kusahau kuwa watoto pia wanawategemea wao katika malezi bora na yanayo faa katika jamii ya watanzania.
Inashangaza kuona mzazi anasema “mimi huyu mtoto amenishinda”. Atakushindaje wakati umemzaa mwenyewe na amekaa miezi tisa tumboni mwako halafu leo uje useme amekushinda? Alihoji mjumbe huyo na kuwataka wazazi waachane na kauli hizo zisizo na maana.
Na: Prisca Japhes.

No comments:

Powered by Blogger.