LIVE STREAM ADS

Header Ads

MTUMISHI WA MUNGU AWATAKA WANANCHI KUCHANGAMKIA FURSA.

Mtumishi wa Mungu Baraka Konisaga ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Baraka Konisaga (Mtumishi wa Mungu) amewataka wakazi wa Jiji la Mwanza na Mkoa wa Mwanza kwa ujumla  kuchangamkia uwepo wa Benki mbalimbali ili kutumia huduma hizo kupata maendeleo.

Akizungumza jana wakati wa uzinduzi wa Tawi la Benki ya Baroda Jijini Mwanza, Konisaga alieleza kwamba Mkoa huu unawafanyabiashara wengi ambao shida yao kubwa ni mtaji na Taasisi nyingi za kifedha hutoza riba kubwa katika mikopo wanayo itoa na kuuasa uongozi wa Benki hiyo kuwepo na unafuu ili waweze kunufaika na huduma zao.

Alieleza kuwa serikali ya awamu ya nne imeweka mikakati mizuri ya kupunguza umaskini kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na kuimalisha ulinzi na usalama katika maeneo mbalimbali na hata katika Baenki zote nchini.

“Pamoja na tawi la Benki ya Baroda kufunguliwa hapa, mjue hapa jijini Mwanza kuna ushindani mkubwa wa huduma za kibenki kwa hali hiyo huduma zenu itabidi ziwe bora ili ziweze kukidhi ushindani uliopo”alieleza.

Konisaga alisema kwamba, wingi wa matawi ya Benki jijini Mwanza ni ushahidi tosha kwamba hali ya ulinzi na usalama ni nzuri na pia hali ya uchumi hususani wa Jiji unakuwa kwa haraka na hivyo kuvutia mabenki mengi kuja kuwekeza hapa nchini.
Na: Prisca Japhes

No comments:

Powered by Blogger.