LIVE STREAM ADS

Header Ads

BARUA YA WAZI KWA WEMA SEPETU.


Kwanza habari yako weye mrembo wa bongo movie najua unaendelea vizuri na sasa upo na mzee wa kitorondo mkifanya yenu.
Dhumuni la barua hii

najua kweli mapenzi ni upofu lakini upofu wako umezidi hata ule wa matonya yaani huwez kuona hata kwa kuhisi .....najua nimekuacha njia panda bado hujajua nazungumzia nini. Ni hayo mahusiano yako na huyo staa wa bongo fleva DIAMOND PLANTINUM

Hivi Wema unajua thaman ya uzuri wako mbona hautendei haki wala hiyo elimu yako nayo bado hujaifanyia kazi. Juzi nikiwa naaangalia tv yangu ya mbao nikakuona nawe kumbe ulikuwepo kwenye fiesta mwanza na wakati diamond anamalizia nyimbo yake ya kitorondo nikakuona nawe ukapanda stejini ukaanza kukatika viuno japo kiuno chako kigumu lakin ulijatahidi kidogo na baadaye ukachukua mic ukaaanza kuongea.

"jaman huyu ananifundisha vitu ambayo mie hata sivijui” Mhhuu hapo moyo wangu ukashituka na kwenda mbali kidogo nikawaza kumbe hivi viuno kakufundisha diamond na hapo nikapata picha Wema ww ulikuwa mpole sana yaan hata muonekano wako na vitu unavyofanya sasa huendani navyo. Ebu mwangalie mwenzieo KLYN na wengine waliopitia level kama zako. Je, wanaishi kama ww? Ndio mali unazo ,elimu unayo sasa kwann unapenda kuteswa na mtu asiyekupenda?

Diamond yupo na ww kwa sababu ya manufaaa yake binafsi, sijui kama hilo unalijua na hivi hajawai kukuomba t*go huyo kweli ebu ngoja nikwambie kitu, raha ya kipele kimpate mkunaji. Ngoja basi Wema nikumalizie hii barua yangu, inaonyesha huyo mzee wa kitorondo anakuomba mengi sana na nawe inaonyesha unakubali bila kizuizi. Hivi kweli hajawai kukuomba t*go maana maneno yako ya siku ile mwanza kwenye fiesta yalinitisha bila aibu ulishika kipaza sauti "jaman huyu ananifundisha mambo mie hata siyawezi”.

Hebu fikiria siku ile alivyokutia aibu pale mlimana city tena kwa upendo tu kwake, japo mligombana lakini ulinyanyuka kwenye kiti kwenda kumtuza pesa, lakini mtoto yule wa kimanyema asivyokuwa na shukran akakuhaibisha mbele za watu maskin na uzuri wako ukatoka kichwa chini kwa aibu.

 

Lakin haikupita miezi mingi nikasikia mmerudiana sikujua alikupa maneno gan matamu mpaka ukalainika. Hebu kumbuka alivyokuponda sana kwenye media kwamba hauna kitu, Kwamba ni yeye na Penina wake tu lakin umesahau yote na sasa upo naye unaonyeha jinsi gani unavyompenda.lakin kumbuka waswahili wanasema penda unapopendwa.Hebu mwangalie Jakline ntabaliwe aka kyln mwenzio hakupenda kuteseka na moyo kaenda kujituliza kwa yule mzee.


Japo wengine wanasema kafuata pesa lakin si unajua waswahili tumeubwa kuongea. Ona walivyotulia na watoto wao mapacha nawe wema ebu soma alama za nyakati.  Umri unaenda achana na hao mabrazamen wasiojali thaman yako, wanakuchezea alafu kesho ukishazeeka wanakuacha.

Hebu muonee tamaa mwenzio Nancy Sumari kaolewa na sasa katulia kwa mumewe, nawe waza kuwa na familia yako na mumeo, huyo brazamen hana nia ya kukuoa ww. Leo naishia hapa maana kalamu yangu imeisha wino ngoje niende dukan nikanunue nitaendelea siku ukipata mume wa kweli.

MWISHO

NB : Kama nimegusa ww shabiki wa wema sorry…

Na: David Chicharito Kagawa.

No comments:

Powered by Blogger.