LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAMLAKA YA HALI YA HEWA NCHINI YASHAURIWA KUBORESHA HUDUMA ZAKE.


Mamlaka ya Hali ya Hewa Hapa nchini (TMA) imeshauriwa kuendelea kuboresha hali ya ufikishaji wa Taarifa za hali ya hewa kwa wananchi, ili
kusaidia kuwaepusha na athari mbalimbali zinazoweza kuwakumba kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.


Ushauri huo umetolewa hii leo Mkoani Mwanza katika Warsha ya Uboreshaji wa huduma za hali ya hewa katika maeneo ya Ziwa Victoria, iliyowahusisha wadau kutoka sekta ya Uvuvi, Kilimo, Usafirishaji wa Majini, SUMATRA na Vyombo vya Habari.

Wakizungumza katika Warsha hiyo, Wadau walioshiriki katika Warsha hiyo ambao pia walishiriki katika Mradi wa Majaribio wa utoaji wa taarifa za utabiri wa hali ya hewa kwa njia ya simu za mkononi wameeleza kuwa, njia ya utoaji wa taarifa za hali ya hewa kwa njia ya simu imewaweza kupata taarifa hizo kwa wakati, ambapo wameiomba TMA kuendelea kuboresha kuwafikishia wa taarifa hizo kwa wakati.


Wadau hao ambao ni Wavuvi na wasafirishaji wa Vyombo vya majini wamesema kuwa, utoaji wa taarifa za utabiri wa hali ya hewa kwa njia ya simu umewasaidia kujiepusha na athari za mabadiliko ya hali ya hewa wawapo katika shughulizao Majini huku wakulima wakibainisha kuwa taarifa hizo zikiendelea kuboreshwa na kuwafikia kwa wakati zitaweza kuwasaidia katika kilimo kwa kuwa wataweza kutambua misimu sahihi shughuli zao.

Aidha Wadau hao wameimbo Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa nchini (TMA) Kuendelea kushirikiana na wadau wengine kama vyombo vya habari, Mitandao ya Kijamii, Mbao za Matangazo kuanzia ngazi za Mitaa na Vijiji pamoja na Mfumo wa njia ya Simu ili kuendelea kutoa taarifa za Utabiri wa hali ya hewa kwa wakati zaidi.

Warsha ya Uboreshaji wa huduma za hali ya hewa katika maeneo ya Ziwa Victoria ambayo imewahusisha wadau mbalimbali wakiwemo wavuvi, Wakulima, Wasafirishaji wa Majini, SUMATRA na Vyombo vya Habari imeanza leo Agost 18 katika Ukumbi wa Hotel ya Gold Crest Jijini Mwanza na inatarajia kufikia tamati kesho kutwa Agost 20 mwaka huu, ambapo warsha hiyo imeandaliwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA.
Monica Mufuri ambae ni Afisa Mawasiliano kutoka TMA.
Wshiriki wa Warsha hiyo.
Wadau wa Huduma za Hali ya Hewa.
Peter Orege Mdau Kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Musoma Mkoani Mara.
Wadau wa Huduma za Hali ya Hewa.
Wadau kutoka Vyombo vya Habari wakiwa Katika Majadiliano.
Wadau wa Huduma za Hali ya Hewa.
Mdau kutoka HHC Alive Radio iliyoko Mkoani Mwanza.
Taswira ya Mkutano ilivyokuwa ndani ya Gold Crest Hotel Jijini Mwanza hii leo.
Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.