LIVE STREAM ADS

Header Ads

WARSHA YA UBORESHAJI WA HUDUMA ZA HALI YA HEWA KATIKA MAENEO YA ZIWA VICTORIA YAFUNGULIWA RASMI JIJINI MWANZA.

Washiriki wa Warsha ya Uboreshaji wa Huduma za Hali ya Hewa katika Maeneo ya Ziwa Victoria kwa Sekta za Uvuvi, Usafirishaji na Kilimo inayoendelea Gold Crest Jijini Mwanza.

Warsha inayohusu Uboreshaji wa Huduma za Hali ya Hewa katika Maeneo ya Ziwa Victoria imefunguliwa Rasmi hii leo Jijini Mwanza, ambapo warsha hiyo imewahusisha wadau kutoka Sekta mbalimbali zikiwemo Uvuvi, Kilimo, Usafirishaji wa Majini, Wanahabari Sanjari na Viongozi mbalimbali.

Warsha hiyo ambayo ilianza jana, imelenga kuboresha hali ya Upatikanaji na Ufikishaji kwa wakati wa Taarifa za Utabiri wa Hali ya Hewa kwa wananchi ili kuwasaidia kujiepusha na athari mbalimbali zinazoweza kuwakumba kutokana na Mabadiliko ya hali ya hewa katika shughuli zao.

Akisoma Taarifa ya Waziri wa Uchukuzi ambae alikuwa Mgeni Rasmi katika, Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Warioba Sanya ambae ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Amewataka Wananchi kuzipokea na kuzifanyia kazi taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) badala ya Kuzipuuzia.

Amesema kuwa Wananchi hususani Wakulima, Wavuvi na Watumiaji wa Vyombo vya Majini wakizifuatilia na kuzizingatia taarifa na utabiri wa hali ya hewa, wataweza kujiepusha na athari zinazoweza kuwakabiri katika shughuli zao kutokana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Warsha ya Uboreshaji wa Huduma za hali ya Hewa Katika Maeneo ya Ziwa Victoria pamoja na mambo mengine, pia imejikita katika majadiliano juu ya Mradi wa Majaribio uliotekelezwa katika Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza, kuhusiana na Utoaji wa Taarifa za Hali ya Hewa kwa njia ya Simu za Mkononi na umenuiwa kuendelezwa katika maeneo yote hapa nchini.


Mradi huo ulianza majaribio yake tangu July 17 mwaka jana, na uliwashirikisha wadau mbalimbali ambao ni pamoja na Wakulima, Wavuvi, Vyombo vya Habari na wasafirishaji wa Majini huku ukiwa umelenga kutumia njia ya simu za mkononi kufikisha taarifa za hali ya hewa kwa wananchi. Warsha hiyo ilianza jana Agost 18 katika Hotel ya Gold Crest Jijini Mwanza, na inatarajia kufikia tamati kesho Agost 20 mwaka huu.
Washiriki wa Warsha hiyo kutoka katika Vyombo mbalimbali vya Habari Mkoani Mwanza, wakiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini TMA.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Mhandisi Warioba Sanya ambae alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo ambae nae alipaswa kumwakilisha Waziri wa Uchukuzi Dk.Harrison Mwanyeke.
Dk.Agness Kijazi ambae ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini TMA .
Dk.Agness Kijazi ambae ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini TMA akiwa katika Mahojiano na Wanahabari.
Dk.Agness Kijazi ambae ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini TMA  (Kulia) akiwa na Maganga ambae ni Mwanahabari kutoka Radio HHC Alive ya Mkoani Mwanza.
Washiriki wa Warsha Hiyo.
Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.