LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATU WANNE WAFARIKI DUNIA JIJINI MWANZA.

Watu wanne wa familia mbiili tofauti wakazi wa mtaa wa Nyerere A, eneo la mabatini jijini Mwanza, wamefariki dunia
usiku wa kuamkia jana baada ya kuangukiwa na mawe wakiwa wamelala.
Tukio hilo limetokea majira ya saa nane usiku, wakati mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali pamoja na radi ilipokuwa ikinyesha.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Nyerere A, mabatini jijini Mwanza, Hassan Maulid amewataja waliofariki dunia kuwa ni Sayi Otieno na Kwinta Kweko ambao ni mume na mke huku watoto wawili Kelfine Masalu na Emanuel Joseph wa familia ya Bw.Joseph William nao pia wakipoteza maisha, baada ya chumba walichokuwa wamelala kuangukiwa na jiwe lililoporomoka kutoka juu mlimani.

Kaimu kamanda wa jeshi la Uokoaji na Zimamoto Mkoa wa Mwanza Inspekta Augustino Magere amewashauri wakazi wa jiji la Mwanza waishio maeneo ya milimani kuchukua tahadhari ili kuepusha maafa kama yaliyojitokeza ikiwa ni pamoja na kuepukana na ujenzi katika maeneo ya milimani ambayo ni hatarishi.
Chanzo: ITV

No comments:

Powered by Blogger.