LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAOMBA MRADI WA JIJI LANGU, SAUTI YANGU UWE ENDELEVU NCHINI TANZANIA.


Wadau mbalimbali wakiewemo wa Serikali naTaasisi binafsi Jijini Mwanza, wameomba Mradi wa Jiji langu, Sauti yangu ambao uliokuwa ukiratibiwa na Mtandao wa Watoto na Vijana Mkoani Mwanza (MYCN) kuwa endelevu baada ya
Mradi huo kufikia tamati.

Mradi huo ambao ulikuwa wa Majaribio katika Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza, Ulianza Majaribio yake tangu Mwaka jana Mwezi wa 12 na Umefikia Tamati Mwaka huu mwezi wa Nane ambapo ulikuwa ukishirikisha makundi mbalimbali.

Makundi hayo yalikuwa ni pamoja na Watoto (Kutoka baraza la watoto Mkoani Mwanza), Vijana (Wa Kike na Kiume), Wanafunzi, Watendaji wa Serikali, Watafiti Vijana Wawakilishi wa Watoto wanaoishi Mitaani na Vyombo vya Habari ambapo ulikuwa umelenga kuchochea mabadiliko ya kimaendeleo miongoni mwa makundi hayo.

Wakizungungumza jana katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa ajili ya kujadili Tathmini ya Mradi huo, Wawakilishi wa Makundi yote yaliyoshirikishwa walishauri kwamba ni vyema mradi huo ukaendelezwa baada ya kuwa majaribio yake yamefikia tamati na kuonekana kuzaa matunda mema.
Wawakilishi wa Watoto kutoka Baraza la Watoto Jijini Mwanza, Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza hilo.

Mradi huo ulikuwa umejikita zaidi kuangalia namna ya kuyashirikisha makundi yaliyotajwa hapo juu kwa lengo la kuleta mabadiliko katika jamii, jambo ambalo washiriki takribani wote wamekiri kwamba limeweza kufanikiwa kwa kuwa mradi huo umeongeza chachu ya mabadiliko kwa wawakilishi wa makundi hayo, chachu ambayo wawakilishi hao wameahidi kuifikisha katika jamii kwa ajili ya kuchochea maendeleo katika jamii.

Hatimae katika Kuhitimisha Kikao hicho, wadau wote kwa ujumla wao wakaomba kwamba Mradi huo unatija kubwa katika jamii, hivyo ni vyema ukaanza rasmi kutekelezwa hapa nchini kwa kuamini kwamba unaweza kuibadili taswira ya Taifa Kimaendeleo.
Wawakilishi wa Wasichana na Wanafunzi Jijini Mwanza.
Mradi wa Majaribio wa Jiji Langu, Sauti yangu ambao ulidumu kwa takribani miezi minane katika Wilaya ya Nyamagana kwa Kujumuisha Kata Nane kati ya 12 za Wilaya hiyo, ulikuwa ukiratibiwa na Shirika la Mtandao wa Vijana na Watoto Mkoani Mwanza (MYCN) kwa Kushirikiana kwa ukaribu zaidi na Shirika la Oxfam na Ulikuwa umelenga kuyashirikisha makundi yote yaliyotajwa ajili ya kujiletea maendeleo katika jamii na Ulikuwa umelenga kuyashirikisha makundi yote yaliyotajwa ajili ya kujiletea maendeleo katika jamii..
Watendaji kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza Mkoani Mwanza.
Mratibu wa Mradi wa Jiji Langu, Sauti Yangu uliokuwa ukiendeshwa na Mtandao wa Watoto na Vijana Mkoani Mwanza (MYCN) Bi.Jessca (Kushoto), akiwa na Katibu Mkuu wa Mtandao huo Brithtius Titus (Kulia).
Mwaakilishi wa Watoto Jijini Mwanza.
Mwaakilishi wa Watoto Jijini Mwanza.
Davis Justine ambae ni Afisa Maendeleo ya Jamii, Idara ya Watoto wanaoishi katika Mazingira Hatarishi kutoka Halmashauri ya Jijini Mwanza.
Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.