LIVE STREAM ADS

Header Ads

GARI LA MBUNGE WA NYAMAGANA LAPIGWA MINYORORO JIJINI MWANZA.


Gari la Mbunge wa Nyamagana Mkaoni Mwanza (Chadema) Mh.Hezekiel Wenje, limepigwa Minyororo na Wakusanya Ushuru wa Vyombo vya Usafiri vinavyoegeshwa katika maeneo ambayo
hayaruhusiwi Kisheria katikati ya Jijini Mwanza.

Gari hilo la Mh.Wenje limefungwa Minyororo hiyo hii jana Ijumaa majira ya saa saba mchana katika eneo la Barabara ya Nyerere mita chache kutoka eneo la Mataa, baada ya Mbunge huyo kuegesha gari lake pembe mwa barabara kwa ajili ya kusalimiana na Wapiga Kura wake katika eneo la Makoroboi.

Baada ya kulifunga minyororo gari hilo, kama kawaida yao wakusanya Ushuru wa Maegesho walisimama pembeni ya gari hilo ili kumsubiria mwenye gari na ndipo walipopigwa na butwaa baada ya kubaini kuwa gari hilo lilikuwa la Mh.Wenje.

Pasipo kujali sheria inasemaje kuhusiana na mtu anaekiuka sheria ya Maegesho, Watoza ushuru hao walilifungua gari hilo bila kuonekana kumueleza Mh.Wenje jambo lolote ikiwa ni pamoja na kumtaka kutoa faini kama ambavyo wamekuwa wakifanya kwa watu wengine ambao wamekuwa wakikamatwa kwa kosa la kupaki katika maeneo yasiyoruhusiwa, ambapo wamekuwa wakiwatoza faini hadi kiasi cha shilingi 50,000.

Kitendo hicho kiliwaacha baadhi ya wananchi wakiwarushiwa watoza ushuru hao maneno ya kuwakebehi kutokana na wao kushindwa kuisimamia kazi yao kwa kufuata sheria inavyowataka, kwa madai kwamba wamekuwa wakifanya kazi kwa kuangaliana usoni.


Wakati baadhi ya wananchi wakisema hayo, baadhi ya wafuasi waliokuwa wamemsindikiza Mh.Wenje ambao wengi wao walikuwa ni Machinga wa Mtaa wa Makoroboi, walisikika wakisema kuwa “Ondoeni hapo uchafu wenu, nyie mnalifunga minyororo hadi gari la Rais wa Nyamagana”?.
Mh.Wenje (Alienyoa) akiwa na Wapiga Kura wake.
Mh.Wenje (Alienyoa) hii leo akiwa na Wapiga Kura wake, wengi wao wakiwa ni Machinga wa Mtaa wa Makoroboi.
Mh.Wenje (Alienyoa) akiwa na Wapiga Kura wake hii leo katika Mtaa wa Makoroboi.
Na Mhariri: Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.