LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMPUNI YA KK-SECURITY GROUP YAWASHANGAZA WATANZANIA.


Kampuni Binafsi ya Ulinzi na Usalama ya KK-Security Group ambayo inafanya shughuli zake za Ulinzi katika nchi mbalimbali barani Afrika ikiwemo Tanzania, Imeendelea kuwashtua watu kwa namna ambavyo
imekuwa na utaratibu wa kutoa Mafunzo kwa Maaskari wake kabla ya Kuwaajiri.                               

Hayo yamebainika hii leo Mkoani Mwanza na baadhi ya Wananchi ambao walifika katika Uwanja Mkongwe wa Nyamagana kushuhudia Maaskari wa Kampuni hiyo waliokuwa wanahitimu Mafunzo yao ya Ukakavu yanayotolewa na Kampuni hiyo.

“Yaani hii Kampuni sijui wao wanawezaje kutoa Mafunzo kwa Maaskari wake kabla ya kuwaajiri. Mbona Kampuni nyingine huwa hazifanyi hivyo? Na kama zipo kampuni zinazofanya hivyo basi ni chache sana” Alieleza mmoja wa Wananchi hao ambae ndugu yake ni Miongoni mwa Maaskari waliohitimu mafunzo hayo.

Baadhi ya Maaskari waliohitimu Mafunzo yao kutoka Katika Kampuni hiyo ya KK-Security wameeleza kuwa, wana imani kubwa na Kampuni hiyo, hivyo wana matarajio makubwa kubwa watakwenda kuitenda kazi yao ipasavyo na kuondokana na suala la ukosefu wa ajira lilliokuwa likiwabili.
Baadhi ya Kampuni za ulinzi hapa nchini, hususani Kampuni binafsi zimekuwa zikilalamikiwa na Maaskari wake kutokana na Ujira Mdogo unaotolewa na Makampuni hayo, huku mengine yakienda mbali zaidi na kuchelesha ama kutotoa malipo kwa wakati kwa maaskari wake hali ambayo ni dhahri kwamba inaweza kuhatarisha usalama katika maeneo yanayolindwa na Makampuni hayo.

Kwa kampuni ya KK-Security, Malalamiko kama hayo hayajasikika yakitolewa hali ambayo imekuwa ikiimarisha uaminifu wa Kampuni hiyo kwa wateja wake na hivyo kujikuta ikijiimarisha siku baada ya siku katika soko la Ulinzi hapa nchini.
Meneja wa KK-Security Kanda ya Ziwa Madam Levina Beal (Kushoto) akiwa Salum  Mwebesa (Kulia) Mmoja wakurugenzi wa Kampuni ya Biashara ya Madini ianayofahamika kama Pamoja Miningi.
Watumishi wa KK-Security.
Waandishi wa Habari waliofika Uwanja wa Nyamagana Mkoani Mwanza kufuatilia Matukio yaliyokuwa yakielendelea uwanjani hapo.
Gwalide la Maaskari wa KK-Security waliohitimu mafunzo yao hii leo katika Uwanja wa Nyamagana Mkoani Mwanza, tayari kwa ajili ya kupangwa katika Vituo vyao vya Kazi.
Na: George Binagi @99.4 Metro FM & Mtanzania Media.

No comments:

Powered by Blogger.